Orchestra Super Mazembe
Orchestra Super Mazembe ilikuwa bendi maarufu nchini Kenya iliyocheza muziki wa Lingala (Soukous). Bendi ilianza na jina la Super Vox , bendi iliyoundwa mwaka 1967 nchini Kongo (kisha Zaire) na kuongozwa na Mutonkole Longwa Didos. Bendi ilihamia Nairobi mwaka 1974 na kubadilisha jina lake kuwa Orchestra Super Mazembe. Kundi hili bado lipo na lilibasilishwa jina na kua Bana Mazembe, Sasa kundi hili linaongwaza na Disco Longwa, mtoto wa Longwa Muntokole Didos.
Kibao chao kikubwa kilikuwa "Shauri Yako", wimbo ulioimbwa mwanzo na Nguashi Ntimbo & Festival Du Zaire. Vibao vingine maarufu ni pamoja na "Samba", "Bwana Nipe Pesa" na "Kassongo". Kundi hili lilisambaratika mwaka 1985.
Super Mazembe inafikiriwa kama mojawapo ya bendi za lingala maarufu sana katika miaka ya 1970/1980 kuwahi kutokea nchini Kenya, pamoja na Les Mangelepa, Baba National ya Baba Gaston na Orchestra Vrunga ya Samba Mapangala.
Wanamuziki wa Bendi
[hariri | hariri chanzo]Kama makundi mengi ya Kongo ya Afrika Mashariki, Super Mazembe daima ilikuwa na mabadiliko ya wanamuziki. Baadhi ya wanamuziki wake walikuwa:
- Mutonkole Longwa Didos (mwimbaji) na kiongozi wa bendi. Alikufa 1999.
- Lovy Longomba (mwimbaji) - Aliacha bendi mwaka 1981 na alianzisha vikundi "Super Lovy" na baadaye "Bana Likasi". Alikufa mwaka 1996. Lovy ni mwana wa Vicky Longomba na nduguye Awilo Longomba, wote wanamuziki maarufu wa Kongo. Wanawe Lovy Christian na Lovi wameunda kikundi Longombas, ambacho ni kikundi maarufu nchini Kenya.
- Kassongo Wa Kanema (mwimbaji) - Aliacha bendi mapema 80'a na kujiunga na Orchestra Virunga. Alikufa 2020
- Loboko Bua Mangala (gitaa la kati). Yeye bado yu hai mpaka leo.
- Kilambe Katele Aley (mwimbaji). Alikufa.
- Bukasa wa bukasa "Bukalos" (gitaa la solo) - Alikufa 1989
- Kayembe Miketo (gitaa) - Alikufa 1991
- Komba Kassongo Songoley (gitaa la kati) - Alikua mpole na mkimya sana. Alikufa 1990
- Kitenge Ngoi wa Kitombole (drum) aka Dodo Doris
- Musa Olokwiso Mangala.
- Atia Jo (Frederick Mulunguluke Mwanza) (gitaa ya besi) - Alifariki 2006 [1]
Diskografia
[hariri | hariri chanzo]LP:
- Mazembe (1980)
- 10 Anniversary (1981)
- Double Gold (1982)
- Kaivaska, (1982) - Virgin Records
- Wabe-Aba (1984)
mkusanyiko:
- Vibao vyao maarufu kabisa (1986)
- Their Greatest Hits
- Maloba D 'Amor (1990) - DiscAfrique
- Vibao vya Mazembe vol. 4
- Vigogo wa Afrika Mashariki (2001) - Earthworks / Stern's Music.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Khayesi, Ajanga. "East Africa Mourns the Death of Veteran Musician Atia Jo", VOA News, Voice of America, 2 Januari 2007. Retrieved on 1 Januari 2009. Archived from the original on 2011-05-23.