Samba Mapangala

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Samba Mapangala
Jina la kuzaliwaSamba Mapangala
AmezaliwaMatadi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
Kazi yakeMwanamuziki

Samba Mapangala alizaliwa mjini Matadi ambayo sasa ni Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Miaka ya awali aliitumia akiwa na bendi mbalimbali huko jijini Kinshasa, kabla kuhamia nchini Uganda mnamo mwaka wa 1975 ambapo yeye na wanamuziki wengine wa Kikongo waliunda bendi ya Les Kinois. Walihamia jijini Nairobi mnamo 1977. Hapa wanaanzisha bendi mpya iliyoitwa Orchestra Virunga, hiyo ilikuwa mwaka 1981. Jina la bendi ni tokeo la milima ya volkeno uliopo huko nchini Kongo maarufu Milima ya Virunga. Orchestra Virunga walitoa albamu yao ya kwanza, It's Disco Time wakiwa na Samba Mapangala mnamo 1982. Mwanzoni mwa miaka ya 1990, kundi likaanza kupata sifa yake ya kimataifa baada ya kutoa albamu zao ya "Virunga Volcano" na "Feet on Fire". [1][2] Mwaka wa kwenye ugawaji wa Tuzo za Kilimanjaro albamu yake Ujumbe ilichaguliwa katika kipengele cha albamu bora ya Afrika Mashariki.[3] Kwa sasa Samba anaishi nchini Marekani.

Diskografia[hariri | hariri chanzo]

Albumu[4]
  • It's Disco Time with Samba Mapangala (1982)
  • Evasion (1983)
  • Safari 1988 (Kenyan cassette)
  • Feet On Fire 1991 (Stern's Africa STCD 1036, CD)
  • Ujumbe 2001 (Stern's / Earthworks STEW43CD)
  • Vunja Mifupa Virunga Roots Volume 1 2004 (Samba Mapangala)
  • Song and Dance (2006) (Virunga Records)
  • African Classics (2008) (Sheer Sound)

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Occidental Brothers: About. Jalada kutoka ya awali juu ya 2018-04-27. Iliwekwa mnamo 2018-03-26.
  2. Richard Trillo: The Rough Guide to Kenya[dead link] 8th Edition, Rough Guides 2006, ISBN 1-84353-651-X
  3. Tanzania Music Awards - Nominees 2004. Jalada kutoka ya awali juu ya 2004-12-04. Iliwekwa mnamo 2004-12-04.
  4. Eastafricanmusic.com: Samba Mapangala and Virunga