Nyumba za wakulima wa Hälsingland

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Nyumba ya kimila ya Hälsingland

Nyumba za wakulima wa Hälsingland (Kiswidi Hälsingegårdar) ni jina la nyumba kubwa za jadi za wakulima katika jimbo la Hälsingland, Uswidi.

Tabia za nyumba za Hälsingland[hariri | hariri chanzo]

Wakulima wa eneo hilo walishindana kujenga nyumba kubwa, mara nyingi za ghorofa mbili, na kuzipamba. Ujenzi ulikuwa wa mbao zinazopatikana kwa wingi katika mazingira hayo yenye misitu minene. Ni nyumba imara maana zinahitaji kudumu katika mazingira ya tabianchi yenye vipindi vya baridi na theluji nyingi pamoja na vipindi vifupi vya joto.

Nyumba zinazopatikana zilijengwa wakati wa karne za 18 hadi 19. Mwaka 2012 nyumba za jadi za wakulima wa Hälsingland zilikubaliwa na UNESCO katika orodha ya Urithi wa Dunia.

Mara nyingi nyumba hizo ziko hatarini maana idadi ya watu wanaolima na kuishi vijijini inapungua.

Orodha[hariri | hariri chanzo]

Nyumba saba zilizotajwa kama urithi wa dunia mwaka 2012 ni zifuatazo[1] :

  • Bommarskatika Letsbo, katika manispaa ya Ljusdal;
  • Erik-Anders, katika Söderala, katika manispaa ya Söderhamn;
  • Fågelsjö gammelgård, katika manispaa ya Ljusdal;
  • Gästgivarskatika Vallsta, katika manispaa ya Bollnäs;
  • Jon-Lars, Alfta, manispaa ya Ovanåker;
  • Kristofers, Järvsö, katika manispaa ya Ljusdal;
  • Pallars, Alfta, manispaa ya Ovanåker.

Nyumba za sanaa[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Kigezo:Lien web.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]