Nenda kwa yaliyomo

Nyumba ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Nyumba ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere ni jumba la makumbusho lililojengwa kwa ajili ya Baba mwanzilishi wa Tanzania Julius Nyerere. Jumba hilo lilijengwa katika kata ya Mzimuni, wilaya ya Kinondoni, Mkoa wa Dar es Salaam, Tanzania. Mtaa wa makumbusho, Kiwanja namba 62, Nyumba namba 2, kata ya Mzimuni.[1]

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Moja ya nyumba ya kwanza ya Mwalimu J.K. Nyerere aliyokuwa nayo wakati wa kupigania uhuru ilikuwa Nyumba ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere iliyopo Magomeni (Sasa ni Mzimuni). Raisi wa kwanza wa Tanganyika aliishi katika nyumba hii wakati wa kupigania uhuru.[1] Nyumba hio ilijengwa na yeye miaka ya 1950 baada ya kujiuzulu kufundisha katika shule ya Mtakatifu Francis, ambayo leo inajulikana kama shule ya Sekondari ya Pugu.[1] Jumba hili lilikuwa mahali kwa ajili ya mikusanyiko na majadiliano ya siri kuhusu mbinu za kukomesha mamlaka ya kikoloni.[1] Nyumba ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere ipo kwenye mtaa uliokuwa makazi ya waanzilishi wengi waliosaidia kuleta uhuru wa nchi, wakiwemo Abasi Kandoro, Amiri Abeid Kalluta, Rashidi Kawawa, Mzee Songambele, Lucy Lameck, John Rupia na wengineo.

  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 https://www.tanzaniaparks.go.tz/uploads/publications/en-1649685096-MWLNYERERE%20ENG.pdf