Nyumba ni Choo (Kampeni)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Nyumba ni Choo ni kampeni ya usafi nchini Tanzania inayosimamiwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii yenye malengo ya kuhamasisha jamii katika kudumisha suala la usafi na ujenzi wa vyoo bora [1].

Kampeni hiyo inafanyika katika wilaya na mikoa mbalimbali ya Tanzania. Ilizinduliwa tarehe 5 Juni 2012 na rais wa awamu ya nne Jakaya Mrisho Kikwete [2] na baadaYe katika awamu ya tano kampeni hiyo ilizinduliwa na aliyekuwa makamu wa rais wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan mwaka 2016.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]