Nenda kwa yaliyomo

Kicheba (ndege)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Nilaus)
Kicheba
Dume la kicheba
Dume la kicheba
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Passeriformes (Ndege kama shomoro)
Familia ya juu: Corvoidea (Ndege kama kunguru)
Familia: Malaconotidae (Ndege walio na mnasaba na mbweta)
Jenasi: Nilaus
Swainson, 1827
Spishi: N. afer
(Latham, 1801)
Ngazi za chini

Nususpishi 10:
N. a. afer
N. a. affinis
N. a. brubru
N. a. camerunensis
N. a. hilgerti
N. a. massaicus
N. a. minor
N. a. miombensis
N. a. nigritemporalis
N. a. solivagus

Kicheba (Nilaus afer) ni ndege katika familia Malaconotidae na spishi pekee ya jenasi Nilaus. Anatokea maeneo makavu kiasi, savana yenye miti hasa. Dume ana utosi mweusi na paji jeupe, mchirizi mweupe juu ya macho na mchirizi mweusi kupitia macho. Mgongo ni mweusi na kidari na tumbo ni nyeupe na mbavu ni kahawianyekundu. Dume wa nususpishi nigritemporalis hana mchirizi mweupe juu ya macho. Jike ni kahawia zaidi wenye michirizi chini. Vicheba hula wadudu katika kanopi ya miti mikubwa. Hujenga tago lao kwa umbo wa kikombe kwa vijiti, manyasi na utando wa buibui katika panda ya mti. Jike hutaga mayai 2.