Newala (mji)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Newala mjini)
Mahali pa Newala (kijani) katika mkoa wa Mtwara.

Newala ni mji na halmashauri katika Mkoa wa Mtwara yenye msimbo wa posta 63401. Mnamo mwaka 2015, mji huo ulikadiriwa kuwa na wakazi 93,728 katika kata 16.[1].

Newala iko karibu na mpaka wa Msumbiji lakini hakuna daraja lililo karibu. Umbali na Mtwara ni km 140, na Masasi km 67. Wakazi wa eneo walio wengi ni Wamakonde, pamoja na Wayao.

Mnamo mwaka 2015 maeneo ya Newala mjini yalipewa halmashauri ya pekee na hivyo kutengwa na Wilaya ya Newala Vijijini[2].

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Makadirio ya Idadi ya Watu katika Majimbo ya Uchaguzi kwa Mwaka 2016, Tanzania Bara, Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dar es Salaam
  2. Historia, tovuti ya Halmashauri ya Mji wa Newala

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Mtwara bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Newala (mji) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.
Kata za Wilaya ya Newala Mjini - Mkoa wa Mtwara - Tanzania

Julia | Luchingu | Mahumbika | Makonga | Makote | Mcholi I | Mcholi II | Mkulung'ulu | Mkunya | Mnekachi | Mtonya | Mtumachi | Namiyonga | Nanguruwe | Nangwala | Tulindane