Bata mzamaji
Mandhari
(Elekezwa kutoka Netta)
Bata mzamaji | ||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||
| ||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||
Jenasi 4:
|
Mabata wazamaji ni ndege wa maji wa nusufamilia Aythyinae katika familia Anatidae. Spishi hizi huzamia kabisa ili kukamata samaki, wanyamakombe au mimea ya maji. Miguu yao iko nyuma zaidi ya mwili kuliko miguu ya mabata wachovya ili kujisogeza mbele vizuri ndani ya maji. Kwa sababu hiyo hawawezi kutembea vizuri. Hutokea kwa makundi kwa maji baridi au milango ya mito, lakini bata mzamaji mkubwa (Aythya marila) huingia bahari wakati wa majira ya baridi. Wanaweza kupuruka sana na spishi za kanda za kaskazini huhamia kusini kila majira ya baridi. Hujenga matago yao visiwani kwa maziwa au ndani ya uoto wa matete uliosongamana.
Spishi za Afrika
[hariri | hariri chanzo]- Aythya affinis, Bata Mzamaji Mdogo (Lesser Scaup)
- Aythya ferina, Bata Kichwa-chekundu (Common Pochard)
- Aythya fuligula, Bata Kishungi (Tufted Duck)
- Aythya innotata, Bata Mzamaji wa Madagaska (Madagascan Pochard)
- Aythya marila, Bata Mzamaji Mkubwa (Greater Scaup)
- Aythya nyroca, Bata Macho-meupe (Ferruginous Duck)
- Marmaronetta angustirostris, Bata Domo-jembamba (Marbled Duck)
- Netta erythrophthalma, Bata Macho-mekundu (Southern Pochard)
- Netta e. brunnea, Bata Macho-mekundu (African Pochard)
- Netta rufina, Bata Utosi-mwekundu (Red-crested Pochard)
Spishi za mabara mengine
[hariri | hariri chanzo]- Aythya americana (Redhead)
- Aythya australis (Hardhead}
- Aythya baeri (Baer's Pochard)
- Aythya collaris (Ring-necked Duck)
- Aythya novaeseelandiae (New Zealand Scaup)
- Aythya valisineria (Canvasback)
- Rhodonessa caryophyllacea (Pink-headed Duck) labda imekwisha
- Netta peposaca (Rosy-billed Pochard)
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Bata mzamaji mdogo
-
Bata kichwa-chekundu
-
Bata kishungi
-
Bata mzamaji wa Madagaska
-
Bata mzamaji mkubwa
-
Bata macho-meupe
-
Bata domo-jembamba
-
Bata macho-mekundu jike
-
Bata utosi-mwekundu
-
Redhead
-
Hardhead
-
Bear's pochard
-
Ring-necked duck
-
New Zealand scaup
-
Canvasback
-
Rosybill