Nenda kwa yaliyomo

Nandy

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Nandy (mwanamuziki))
Nandy
Picha ya Nandy
Nandy juu ya jukwaa la Tamasha la Fiesta mjini Dodoma, Tanzania, 2017
Taarifa za awali
Jina la kuzaliwaFaustina Charles Mfinanga
Amezaliwa(1992-11-09)Novemba 9, 1992 (age 33)
Mawenzi, Moshi, Tanzania
Kazi yake
Miaka ya kazi2010–hadi sasa

Nandy (amezaliwa Kilimanjaro, Tanzania, 9 Novemba, 1992) ni mwimbaji na mtunzi wa nyimbo kutoka nchini Tanzania.

Mnamo mwaka 2017 alishinda tuzo ya All Africa Music Awards katika kundi la wasanii bora wa kike kutoka Afrika Mashariki.[1][2]

Maisha ya awali

[hariri | hariri chanzo]

Nandy alizaliwa na Mary Charles, fundi cherehani na Charles Mfinanga, ambaye ni fundi makenika. Jina la Nandy ni kifupi cha jina lake halisi Nandera. Alianza kutumbuiza akiwa na umri mdogo kabisa. Akiwa na miaka mitano, alikuwa mwanachama hai wa kwaya ya mafunzo ya Jumapili ya Kanisa la KKKT huko Moshi. Alimaliza elimu ya msingi katika shule ya msingi ya Mawenzi, baadaye alijiunga Lomwe High School ambako huko alikuwa mwana-kwaya mkuu katika shule hiyo. Baada ya kumaliza elimu ya juu alijiunga na Chuo cha Biashara (CBE), Dar es Salaam, Tanzania.

Tanzania House of Talent

[hariri | hariri chanzo]

Kazi yake ilianza kujulikana baada ya rafiki yake kumtambulisha kwa marehemu Ruge Mutahaba, aliyekuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania House of Talent (THT). Hapa ndipo alipokutana na Ema the Boy, ambaye ndiye aliyekuja kumtayarishia kibao chake maarufu cha Nagusagusa. Wimbo uliokuja kutamba mno wiki tu tangu kutolewa kwake.

Mwanzoni mwa mwaka wa 2016 alishiriki kwenye mashindano ya kuimba yaliyoandaliwa na Tecno. Shindano lilishirikisha washiriki wengine kutoka nchi kibao za Afrika na kipindi cha fainali kilichofanyika huko Lagos, Nigeria, Nandy aliibuka kama mshindi wa pili. Shindano hili lilimkuza kimuziki, hasa katika suala zima la utumbuizaji jukwaani, alipata maarifa ya muhimu kutoka kwa magwiji wa muziki kama vile akina M.I Abaga, Yemi Alade na Bien wa Sauti Sol.[3][4]

Mwaka 2017 alitoa kibao cha One Day ambacho kilisukuma kazi yake na hatimaye kumpa nafasi kadhaa zilizomfanya kushiriki kwenye Coke Studio Africa 2017 na mwaka huohuo akaja kuchaguliwa kwenye tuzo za All Africa Music Awards katika kundi la wanamuziki bora wa kike kutoka Afrika Mashariki na kuibuka mshindi na akatoa kibao kiitwacho kivuruge na hivi sasa anatamba na wimbo wake ambao amefanyakazi yeye na willy paul ambao jina lake ni hallelujjah[5][6][7][8][9]

Mbali na muziki, yeye ni mpenda mitindo na ndiye mmiliki wa Prints by Nandy Africa. Yeye pia ni balozi wa UNICEF, mwanamitindo wa nguo za harusi za kina dada na miliki wa Make up by Nandy.[10]

  • African Princess (2018)[11]
  • I'm Confident (2013)
  • Nagusa gusa (2017)
  • One Day (2017)[12]
  • Wasikudanye (2017)
  • Kivuruge (2017)[13]
  • Ninogeshe (2018)[14]
  • Antena 2024

Tuzo na chaguzi

[hariri | hariri chanzo]
Mwaka Shere ya Tuzo Tuzo Mpokeaji Tokeo
2017 All Africa Music Awards[1][2] Msanii Bora wa Kike Afrika Mashariki Nandy Ameshinda
2018 AMI Awards Afrika[15] Msanii Bora Chipukizi Nandy Pending
  1. 1 2 "AFRIMA 2017: Full list of winners". Music In Africa (kwa Kiingereza). 2017-11-13. Iliwekwa mnamo 2018-05-12.
  2. 1 2 Azaniapost. "Bongo Flava: Ali Kiba, Nandy win awards at AFRIMA in Nigeria". Azaniapost (kwa Kituruki). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-07-29. Iliwekwa mnamo 2018-05-12. {{cite news}}: More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help)
  3. "29-year-old wins $25K, recording deal". pulse.ng (kwa American English). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-06-27. Iliwekwa mnamo 4 Mei 2018.{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. "Tanzania: Heartbreak for Tanzania's Nandy in Lagos". allafrica.com (kwa American English). Iliwekwa mnamo 4 Mei 2018. {{cite news}}: Unknown parameter |subscription= ignored (|url-access= suggested) (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. "MEET THE AFRICAN PRINCESS". coca-cola.co.ke. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-08-14. Iliwekwa mnamo 4 Mei 2018.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  6. "Nandy: Mane Fitsum (Cover) - Coke Studio Africa". coca-colacompany.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-06-27. Iliwekwa mnamo 4 Mei 2018.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  7. "Aslay – Subalkheri Mpenzi Ft Nandy". celebvibestar.co.ke. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-06-27. Iliwekwa mnamo 4 Mei 2018.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  8. "Coke Studio Africa 2017 Officially Launches In Ethiopia". ethiosports.com. Iliwekwa mnamo 4 Mei 2018.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  9. "Nandy and AliKiba shine at Afrima". thecitizen.co.tz. Iliwekwa mnamo 4 Mei 2018.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  10. https://mdundo.com/news/31026
  11. "The African Princess | Mistari Yetu: Albamu ya Nandy The African Princess". Mistari Yetu (kwa American English). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-10-31. Iliwekwa mnamo 2019-09-10.
  12. "Nandy – One Day". notjustok.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-06-27. Iliwekwa mnamo 4 Mei 2018.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  13. "New Music: Nandy – Kivuruge". uplandradiofm.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-05-05. Iliwekwa mnamo 4 Mei 2018.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  14. "Nandy – Ninogeshe". tooxclusive.com.ng. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-06-27. Iliwekwa mnamo 4 Mei 2018.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  15. "AMI Awards Afrika 2018 full nominee list". whatshappeningmagazineug.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-07-31. Iliwekwa mnamo 4 Mei 2018.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
  1. Nandy: Youtube
  2. Nandy: MistariYetu Ilihifadhiwa 23 Oktoba 2019 kwenye Wayback Machine.