Nakaaya
Nakaaya | |
---|---|
Nakaaya akiwa katika pozi
| |
Maelezo ya awali | |
Jina la kuzaliwa | Nakaaya Abraham Sumari |
Amezaliwa | 3 Septemba 1982 |
Asili yake | Arusha, Tanzania |
Aina ya muziki | R&B, Hip hop, dansi |
Kazi yake | Rapa |
Ala | Sauti |
Miaka ya kazi | 2004 - hadi leo |
Studio | 41 Records |
Tovuti | Tovuti ya Nakaaya |
Nakaaya Abraham Sumari (anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama Nakaaya tu; amezaliwa 3 Septemba 1982, Arusha mkoa wa Kaskazini mwa Tanzania) ni mwimbaji wa muziki wa R&B, Hip hop, na dansi kutoka nchini Tanzania.
Anajulikana sana kwa kibao chake mashuhuri cha Mr. Politician. Huyu ni dada ya aliyekuwa mrembo wa Tanzania kwa mwaka wa 2005, Nancy Sumari.
Wasifu
[hariri | hariri chanzo]Maisha ya awali
[hariri | hariri chanzo]Yeye ni wa kwanza kuzaliwa kutoka katika familia ya watoto watano. Wazazi wake ni wafanyabiashara huko mkoani Arusha. Nakaaya alikulia mjini Arusha na Nairobi, Kenya, ambapo alikwenda kwa sababu za kimasomo. Akiwa bado yungali mdogo, Nakaaya alipenda sana kuimba na kutumbuiza.
Baada ya kumaliza shule, alihamia jijini Dar es Salaam na akawa anafanya kazi katika nyanja kadhaa za kitawala kabla hajajiendeleza na masuala ya kimuziki. Nakaaya alishawahi kufanya kazi na bendi ya Tanzanite ambao walimwalika ili wafanyenaye kazi kunako mwaka wa 2004. Lakini, ilimlazimu kusimamisha shughuli za muziki kwa muda ili isije ikaingliana na kazi zake za kila siku.
Mnamo mwaka wa 2006, akapata nafasi katika moja kati ya matamasha ya Tusker Project Fame ambayo yalifanyika katika jumba la Dar Cinemas. Nakaaya akapata bahati ya kumvutia mmoja wa wa majaji kwa uwezo wake na kipaji alichonacho. Hivyo akawa mmoja kati ya waamuru katika kipindi hicho.
Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]- Nakaaya katika Tanzania Directoty.info
- Tovuti Rasmi ya Nakaaya Archived 22 Machi 2007 at the Wayback Machine.
Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Tanzania bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Nakaaya kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |