Nancy Sumari

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Katika kigezo hiki unataja tarehe YYYY|MM|DD maana yake ni 1999|10|24 kwa maana "24 Oktoba 1999"

Nancy Sumari
Miss-africa2.jpg
Nancy akiwa na Mama Salma Kikwete.
Amezaliwa 7 Agosti 1986 (1986-08-07) (umri 33)
Arusha
Nchi Tanzania
Kazi yake Mwanamitindo
Taji Miss Tanzania 2005
Ndugu Nakaaya

Nancy Abraham Sumari alikuwa Mrembo wa Tanzania kwa mwaka 2005 na pia alikuwa Mrembo wa Dunia wa Afrika kwa mwaka 2005. Nancy Sumari alizaliwa tar. 7 Agosti mwaka 1986 mkoani Arusha Tanzania, na kupata elimu yake ya msingi mjini Nairobi, Kenya katika shule ya msingi ya Blue Bells. Baadaye kuingia elimu ya Sekondari ya wanawake ya Maasai ya huko huko Nairobi’NBO’ na kuhitimu mwaka 2004 na baadae kujiunga na Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam akisomea masuala ya utawala wa biashara .

Maisha binafsi[hariri | hariri chanzo]

Nancy ni mtoto wa tatu katika familia ya Mzee Abraham Simango Sumari, akiwa na dada yake Glory alyekuwa anampa hamasa na ushauri zaidi juu ya masuala ya urembo. Ndugu zake wengine katika ukoo wao ni Devis, Patra, Tumo na Nakaaya Sumari.

Taji Alichukua[hariri | hariri chanzo]

Tarehe 2 Septemba mwaka 2005 Alichaguliwa kuwa Mrembo wa Tanzania kwa mwaka 2005.

People.svg Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Nancy Sumari kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.