Nenda kwa yaliyomo

Nagasaki

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Nagasaki, Nagasaki)
Nagasaki mwaka 2004.
Mahali pa Nagasaki.

Nagasaki ni mji wa Japani kwenye kisiwa cha Kyushu mwenye wakazi 450,000.

Umejulikana kimataifa kwa sababu uliharibiwa tarehe 9 Agosti 1945 na bomu la nyuklia la Kimarekani kama mji wa pili katika historia baada ya Hiroshima. Bomu hilo liliua watu 36,000 mara moja na wengine waliokadiriwa kuwa kati ya 70,000 na 100,000 walikufa baadaye kufuatana athari ya mnururisho wa kinyuklia.

Kihistoria Nagasaki ilikuwa kitovu cha Ukristo katika Japani mnamo mwaka 1600. Imani hiyo ilipigwa marufuku na serikali, hivyo Wakristo wengi waliuawa katika miaka iliyofuata. Wachache walitunza imani kwa siri hadi kurudishwa kwa uhuru wa dini katika karne ya 19.

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]
WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu maeneo ya Japani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Nagasaki kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.