Nabii Gadi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Nabii Gadi alikuwa nabii wa Israeli wakati wa Mfalme Daudi (mnamo mwaka 1000 KK hivi).

Unabii wake[hariri | hariri chanzo]

Habari zake zinapatikana katika Biblia, kuanzia 1Sam 22:5, alipomuambia Daudi arudi nchini Yuda.

Habari muhimu zaidi ni utabiri wa adhabu ambao Gadi alimfanyia kutokana na kosa la kupiga sensa ya wanaume wa utawala wake (2Sam 24:11-13). Kwa niaba ya Mungu alimuachia achague mwenyewe moja katika ya balaa tatu.

Gadi anatajwa kwa mara ya mwisho katika 2Sam 24:18, alipomuagiza Daudi amjengee Mungu altare ili tauni aliyojichagulia ikome.

1Nya pia inasimulia habari zake na katika 29:29 inataja kitabu chake kilichopotea.

Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Nabii Gadi kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.