Nenda kwa yaliyomo

Mwananchi Communications

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Mwananchi Communications Ltd ni kampuni nchini Tanzania. Inajishughulisha na uchapishaji wa mdeia na vyombo vya habari vya kidijitali. Kampuni hii ni wachapishaji wa gazeti maarufu la Kiswahili la kila siku Mwananchi na mengine kama vile The Citizen, Sunday Citizen, Mwananchi Jumapili, Mwananchi Scoop na Mwanaspoti .

Mhariri mtendaji ni Victor Mushi na mhariri mtendaji wa gazeti la Mwananchi ni Joseph Nyabukika. Michael Momburi anaongoza Mwanaspoti nchini Tanzania na Kenya. Sanga, aliyekuwa Mhariri Mtendaji anachukuliwa kuwa gwiji wa uandishi wa habari za michezo.

Mpoki Thomson ni Mhariri Mkuu wa magazeti ya The Citizen na Sunday Citizen, ambayo yamechangia katika mabadiliko ya kijamii na kiuchumi nchini Tanzania.Baada ya kuteuliwa kwa jukumu la Mhariri Mkuu mnamo Januari 2021, alikua mhariri kijana zaidi kushikilia wadhifa kama huo akiwa na umri wa miaka 28.

Bakari Machumu, ambaye aliwahi kuwa Mhariri Mtendaji sasa ni Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo.

Mwananchi Communications Limited ilianzishwa Mei 1999 na Ferdinand Ruhinda [1] kwa jina la Media Communications Ltd. Lakini Aprili 2001, biashara mpya ilianzishwa (Advertising Agency & Public Relations) na kampuni mpya ya Mwananchi Communications Ltd ikaanzishwa. Katika mwaka huo huo Mwananchi Communications Ltd ilinunuliwa [2] [3] na Nation Media Group [4] (NMG), ambayo iko Nairobi, Kenya . [5]

Makao yake makuu yapo katika Kiwanja Na. 34/35 Tabata Relini [6] kwenye Barabara ya Mandela, Dar es Salaam, Tanzania . [7]

Historia[hariri | hariri chanzo]

Historia ya Kampuni ya Mwananchi Communications Ltd ilianza kwenye mwaka 1999 ambapo Ferdinand Ruhinda [1] alianzisha kampuni ya mawasiliano ijulikanayo kama Media Communications Ltd, ambayo ilianzisha gazeti la kila siku la Kiswahili Mwananchi lililosajiliwa Aprili 20, 2000.

Tarehe 27 Mei, 2000, nakala ya kwanza ya Mwananchi ilizinduliwa. Lilikuwa gazeti la kurasa 12 lililouzwa kwa TSh150. Soko la wakati huo lilikuwa na magazeti matatu pekee ya kila siku ya Kiswahili.

Muda mfupi baada ya kuzinduliwa kwa Mwananchi, gazeti la michezo la kila wiki la Mwanaspoti lilizinduliwa Februari 12, 2001. Ilikuwa gazeti la kurasa 12 lililouzwa kwa Sh100 pekee.

Baada ya kusajili gazeti la The Citizen mnamo Machi 2, 2001, gazeti hili lilizinduliwa kikamilifu na kuchapishwa Septemba 16, 2004, na kuwa gazeti la tano la kila siku la Kiingereza sokoni.

Magazeti ya kampuni yalichapishwa kwa mkataba hadi 2005, ilipopata mashine ya uchapishaji ya mitumba kutoka Australia.

Mwaka 2020, chini ya serikali ya rais Magufuli, kampui iliamriwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania kusitisha uchapishaji wa gazeti la Mwananchi mtandaoni kwa muda wa miezi sita na kulipa faini ya shilingi milioni 5 kwa kuchapisha "taarifa za upotoshaji zilizosababisha mkanganyiko katika jamii". [8] Wafanyakazi wawili walikamatwa na kushtakiwa kwa kukiuka sheria ya uhalifu wa mtandao ya 2015 . [9]

Magazeti[hariri | hariri chanzo]

Magazeti ya Kiingereza
 • The Citizen – Gazeti la Kiingereza nchini Tanzania
 • The Citizen on Sunday - Toleo la Jumapili la The Citizen
Magazeti ya Kiswahili
 • Mwananchi – gazeti la kila siku nchini Tanzania
 • Mwanaspoti – Gazeti la michezo na burudani linalotoka kwa wiki mbili
 • Mwanaspoti Kenya - Gazeti la kwanza la michezo la Kiswahili nchini Kenya
 • Mwananchi Jumapili – Toleo la Jumapili la gazeti la Mwananchi
 • Mwananchi Scoop - Jarida la kidigitali la Swanglish kwa vijana, hasa wanfuzi wa vyuo, linaloangazia hadithi za burudani na michezo, hadithi, masengenyo, taaluma na ujuzi, teknolojia, afya, mitindo na usimamizi wa pesa.

Majarida[hariri | hariri chanzo]

Majarida ya Kiingereza
 • Your Health- gazeti la afya linalochapishwa kila Jumatatu na kubebwa katika The Citizen
 • Political Platform - jarida la mapitio ya kisiasa linalochapishwa kila Jumatano na kubebwa katika The Citizen
 • Success - jarida la mapitio ya elimu linalochapishwa kila Jumatatu na kuwekwa katika The Citizen
 • The Beat – jarida linaloangazia masuala ya burudani na showbiz inayochapishwa kila Ijumaa na kubebwa katika The Citizen
 • Business Week - jarida la biashara linalochapishwa kila Alhamisi na kubebwa katika The Citizen
 • Woman – gazeti la mwanamke linalochapishwa kila Jumamosi na kubebwa katika The Citizen
 • Sound Living - Jarida la familia ambalo huangazia hadithi za kusisimua zinazotokea katika jamii
Majarida ya Kiswahili
 • SpotiMikiki – jarida la michezo linalochapishwa kila Jumatatu na kuwekwa katika Mwananchi
 • Siasa – inakazia uchambuzi wa matukio ya kisiasa; linalochapishwa kila Jumanne na kuwekwa katika Mwananchi
 • Maarifa – inalenga wanafunzi na walimu. Inalochapishwa kila Jumatano na kuwekwa katika Mwananchi
 • Uchumi – jarida linaloenga habari za biashara, matukio na mambo ya kiuchumi; linachapishwa kila Alhamisi na kuwekwa katika Mwananchi
 • Jungukuu – jarida la kijamii linalochapishwa kila Jumamosi na kuwekwa katika Mwananchi
 • Starehe – jarida la michezo linalochapishwa kila Jumamosi na kuwekwa katika Mwananchi
 • Johari – jarida la pekee linalolenga wasomaji wa kike linalochapishwa kila Jumapili na kuwekwa katika Mwananchi Jumapili

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

 1. 1.0 1.1 "Rostam Aziz of New Habari Corporation: The facts". Jamiiforums.com. Iliwekwa mnamo 2014-04-16. Hitilafu ya kutaja: Invalid <ref> tag; name "jamiiforums1" defined multiple times with different content
 2. "Nation Media Group moves into Tanzanian market - AP Worldstream | HighBeam Research". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Novemba 3, 2012. Iliwekwa mnamo 2010-04-06.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
 3. "ICT Hall of Fame • Wilfred Kiboro". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Juni 13, 2010. Iliwekwa mnamo 2010-04-06.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
 4. Accessmylibrary.com http://www.accessmylibrary.com/article-1G1-95414770/kenya-nation-media-group.html. Iliwekwa mnamo 2014-04-16. {{cite web}}: Missing or empty |title= (help)
 5. "Nation Media Group Limited - Company Snapshot". www.alacrastore.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 31 Julai 2012. Iliwekwa mnamo 2 Februari 2022.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
 6. "Wikimapia - Let's describe the whole world!". wikimapia.org. Iliwekwa mnamo 2017-08-23.
 7. "Mwananchi Communications Ltd - Dar es Salaam - Media/Nieuws/Publicaties". Facebook. Iliwekwa mnamo 2014-04-16.
 8. "TCRA suspends Mwananchi's online license for six months". The Citizen. 17 Aprili 2020. Iliwekwa mnamo 22 Januari 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
 9. "News: Wafanyakazi 2 wa gazeti la Mwananchi mbaroni kwa upotoshaji". Muakilishi (kwa swahili). 2 Mei 2020. Iliwekwa mnamo 22 Januari 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: unrecognized language (link)