Muthoni Gathecha

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Muthoni Gathecha (alizaliwa tarehe 8 Aprili 1962) ni mwigizaji wa kike wa filamu kutoka Kenya. Alishiriki katika tamthilia tofauti za televisheni nchini Kenya.[1]

Maisha ya awali[hariri | hariri chanzo]

Muthoni ni mkufunzi na mkuu wa taaluma katika Chuo Kikuu cha Kenyatta. Alipata mafunzo ya uwanasaikolojia kutoka Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Marekani.[1]

Kazi[hariri | hariri chanzo]

Mwaka 2013, alikua miongoni mwa wahusika wakuu wa telenovela ya Kenya kwa jina la Kona. Aliigiza pamoja na washiriki kama Nini Wacera, Janet Sision, na Lwanda Jawar.[2][3] Baadaye alirudi katika televisheni mwaka 2014 alipokua mhusika mkuu katika filamu ya Pray and Prey kama Margaret, mama muovu. Ushiriki wake wa hivi karibuni ni katika telenovela kwa jina la Skandals kibao, ambapo aliigiza kama mama mwenye upendo kwa binti zake wawili. Aligawana sifa na waigizaji Avril na Janet Sision.[4] Amejitokeza hasa katika filamu zilizoongozwa chini ya Africa Magic Movie Franchise. Inahusisha filamu kama Shortlist, Close Knit Group, Get Me a Job, The Black Wedding, The Next Dean, na I Do.

Maisha binafsi[hariri | hariri chanzo]

Muthoni ni mama wa watoto watatu. Mtoto wake wa kwanza ni mwanamuziki maarufu kwa jina la Mchizi Gaza. Mwanae wa pili Rowzah ni mwanamitindo. Kitindamimba ni Mizen.[1]

Filamu[hariri | hariri chanzo]

Mwaka Kazi Uhusika Kichwa
Televisheni
2013 Kona Ariya Oyange Mhusika Mkuu [5]
2014-15 Pray and Prey Margaret Mpinzani Mkuu [6]
2015–present Skandals kibao Mama Mhusika Mkuu
2015–present "Mama digital" mama wa digitali jukumu la kiuongozi

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. 1.0 1.1 1.2 "Muthoni Gathecha's biography". actors.co.ke. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-02-23. Iliwekwa mnamo October 30, 2015.  Check date values in: |accessdate= (help)
  2. "Kona new series". velasign.com. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-03-04. Iliwekwa mnamo October 29, 2015.  Check date values in: |accessdate= (help)
  3. "Muthoni Gathecha in Kona". kenyabuzz.com. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-03-10. Iliwekwa mnamo October 30, 2015.  Check date values in: |accessdate= (help)
  4. "Skandals kibao". talenteastafrica.com. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-10-02. Iliwekwa mnamo October 30, 2015.  Check date values in: |accessdate= (help)
  5. "Kenya telenovela panks a punch". beta.iol.co.za. Iliwekwa mnamo October 29, 2015.  Check date values in: |accessdate= (help)[dead link]
  6. "The social client pray and prey". socializeltd.com. Iliwekwa mnamo October 30, 2015.  Check date values in: |accessdate= (help)[dead link]