Murder Was the Case

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Murder Was the Case
Murder Was the Case Cover
Soundtrack ya Wasanii mbalimbali
Imetolewa October 15, 1994
Imerekodiwa 1993-1994
Aina West Coast Hip Hop, G-Funk, Rap
Urefu 68:30
Lebo Death Row/Interscope
Mtayarishaji Dr. Dre
Dat Nigga Daz
Sam Sneed
Soopafly
DJ Quik
Devante Swing
Makadirio ya kitaalamu
Tahakiki za ushindi
Chanzo Makadirio
Allmusic 4.5/5 starsStar full.svgStar full.svgStar full.svgStar half.svg[1]

Murder Was the Case ni jina la kutaja filamu na albamu ya kibwagizo kifupi cha mwaka wa 1994 ambacho kimechezwa na Snoop Doggy Dogg. Filamu hii yenye urefu wa dakika 18 iliongozwa na Dr. Dre na Fab Five Freddy ikiwa na wendo wa hadithi ya kifo cha Snoop Dogg na kufufuka kwake baada ya kuingia mkataba na Shetani. Jina la filamu linatokana na wimbo wa Snoop ambao upo katika albamu yake ya kwanza, Doggystyle, ambao ulitoka mapema kabla ya filamu hii. Albamu ilishika nafasi ya kwanza kwenye chati za Billboard 200 mnamo Novemba 5, 1994 ikiwa na mauzo yapatayo 329,000 katika wiki yake ya kwanza na vilevile ilipata kutamba katika chati za albamu Top R&B/Hip-Hop.

Wiki iliyofuata ilikaa nafasi ya juu ikiwa imeuza nakala 197,000 na kupewa hadhi ya Dhahabu. Albamu ilitunukiwa hadhi ya platinum 2x ikiwa na mauzo ya nakala 2,030,000. Wimbo wa "What Would You Do" iliingizwa katika kibwagizo cha Natural Born Killers na kilipata kichaguliwa kwenye Grammy Award for Best Rap Performance by a Duo or Group katika sherehe za ugawaji wa tuzo hizo mnamo 1996. Albamu ilitolewa tena ikiwa na DVD ya ziada yenye video 3 mnamo 11 Julai, 2006.

Tupac Shakur alilipwa $200,000 na mmiliki wa Death Row Records Suge Knight kurekodi wimbo kwa ajili ya albamu hii. Wimbo ulirekodiwa, lakini haujatumika katika toleo halisi la kibwagizo. Udaku ulioenea kuhusu rekodi yenyewe ni kati ya "Pain" ambao baadaye ulikuja kutumika kwa ajili ya kibwagizo cha filamu ya Above The Rim, "High Til I Die Interscope Version", ambao baadaye ulitolea upya na kutumika kwa ajili ya albamu ya Sunset Park wakati 2Pac yupo katika studio ya Death Row Records, na Unreleased Version Of R U Still Down. R U Still Down ni sawa na toleo ambalo lilitolewa mnamo 1997 katika albamu ya 2Pac ya "R U Still Down". Hata hivyo, wimbo una biti tofauti, beti ya kwanza ambayo awali haikuwepo, kiitikio cha kike, na beti ya pili na tatu ambazo zimerekodiwa upya ambazo pia zinafanana kabisa na beti 1-2 ya kwenye toleo la albamu ya R U Still Down.

Mapokezi[hariri | hariri chanzo]

Orodha ya nyimbo[hariri | hariri chanzo]

# Jina Mwimbaji (wa) Mtayarishaji (wa)
1 "Murder Was the Case" (Remix) Snoop Dogg Dr. Dre
2 "Natural Born Killaz" Dr. Dre; Ice Cube Dr. Dre; Sam Sneed
3 "What Would U Do" Tha Dogg Pound; Snoop Dogg Dr. Dre; Dat Nigga Daz
4 "21 Jumpstreet" Snoop Dogg; Tray Deee Dat Nigga Daz
5 "One More Day" Nate Dogg featuring Nanci Fletcher Dat Nigga Daz
6 "Harvest for the World" Jewell Dr. Dre
7 "Who Got Some Gangsta Shit?" Snoop Dogg; Tha Dogg Pound; Lil' C-Style; Swoop G Soopafly
8 "Come When I Call" Danny Boy DJ Quik
9 "U Better Recognize" Sam Sneed; Dr. Dre Sam Sneed; Dr. Dre
10 "Come Up to My Room" Jodeci; Tha Dogg Pound Dat Nigga Daz; Devante Swing
11 "Woman to Woman" Jewell DJ Quik; G-One
12 "Dollaz + Sense" DJ Quik DJ Quik
13 "The Eulogy" Slip Capone; CPO Sam Man
14 "Horny" B-Rezell Kevin Lewis; Marc McWilliams
15 "Eastside-Westside" (Remix) Young Soldierz Big Wy; Lil' Stretch
16 "Hot One" (wimbo wa ziada kwa ajili kanda za kaseti tu) O.F.T.B. O.F.T.B.

Sampu[hariri | hariri chanzo]

21 Jumpstreet

Who Got That Gangsta Shit"

Come When I Call

Woman to Woman

Dollaz & Sense

  • "I Like (What You're Doing to Me)" wa Young & Company

Eastside-Westside

Single[hariri | hariri chanzo]

Nafasi za chati[hariri | hariri chanzo]

Album - Billboard (North America)

Mwaka Chati Nafasi
1994 The Billboard 200 1

Washika dau[hariri | hariri chanzo]

  • Mtayarishaji Mtendaji: Suge Knight
  • Mkuu wa sauti: Dr. Dre
  • Mkaguzi: Dat Nigga Daz.
  • -Merekodiwa katika Can-Am Studios
  • Imechanganywa katika studio za Dr. Dre
  • Wahandisi wa Death Row: Kesten Wright, Tommy D. Daugherty na Danny Alfonso.
  • Wapiga picha: Yoko Sato, Simone Green

Waliorudia[hariri | hariri chanzo]

  • Jeremy Messersmith akiwa na Andy Thompson aliimba wimbo wa "Murder Was the Case" kwenye The Cake Shop huko mjini Minneapolis, MN kwa ajili ya wazo la tamasha la 'Murder and Death' mnamo 1/10/2010.
  • Don Vito and Mad DPS walitoa toleo lao 2008 katika albamu ya nyimbo mchanganyiko ya 'The Triple-Six Mixtape.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Vingo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Murder Was the Case at the Internet Movie Database