Mtumiaji:Tatianna20/Utetezi wa watoto
Utetezi wa watoto ni mpango mkakati ulioanzishwa kwa ajili ya kuwawezesha watoto kuwa kundi la watu ambao wamepewa nguvu ya kupambana na ubaguzi baina ya watoto au sifa za watoto.[1] Kwa hivyo mpango huu unaweza kufanya kazi kama istilahi chanya, kama vile neno ufeministi, na pia neno muhimu kubainisha jambo fulani, kama neno ubaguzi wa rangi. Dhana ya mwisho inajulikana zaidi kama umri, utu uzima au mfumo dume.Dhana hii ilielezewa kwa mara ya kwanza na kuchunguzwa katika makala ya Chester M. Pierce na Gail B. Allen mwaka wa 1975.[2] Ilitumiwa kwa muda katika miaka ya 1990 katika nadharia ya fasihi na Peter Hunt kurejelea "kusoma kama watoto."[3] Katika uwanja wa masomo ya utotoni, na kwa kawaida katika Ulaya, utetezi wa watoto ni jambo chanya kulingana na kazi ya John Wall tangu 2006 na kitabu, Ethics in Light of Childhood. Tabia ya malezi ya mtoto kama jambo hasi yanapatikana katika kitabu cha mwisho cha Elisabeth Young-Bruehl, kilichochapishwa baada ya kifo chake, Childism: Confronting Prejudice Against Children.[4]
Hivi karibuni, Taasisi ya Utetezi wa watoto imeanzishwa katika Chuo Kikuu cha Rutgers Camden, Marekani, ikifanya mkutano wake wa kwanza tarehe 11 Juni 2020. Taasisi ya Utetezi wa watoto ni mtandao wa utafiti wa kimataifa na watetezi wanaojitolea "kuwawezesha watoto kwa kukosoa kanuni na miundo [ya watu wazima]".[5] Pamoja na mambo mengine, Taasisi ya Utetezi wa watoto inahifadhi kanzidata ya utafiti ambayo aidha inatumia dhana ya utetezi wa watoto au inaendana nayo kwa karibu.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ https://en.wiktionary.org/wiki/childism
- ↑ https://journals.healio.com/doi/10.3928/0048-5713-19750701-04
- ↑ amazon.com/Criticism-Theory-Childrens-Literature-Peter/dp/0631162313
- ↑ https://www.google.com/search?q=Young-Bruehl%2C+Elisabeth+(2012).+Childism%3A+Confronting+Prejudice+Against+Children.+Yale+University+Press.&rlz=1C1KNTJ_enTZ1032TZ1032&oq=Young-Bruehl%2C+Elisabeth+(2012).+Childism%3A+Confronting+Prejudice+Against+Children.+Yale+University+Press.&aqs=chrome.0.69i59.1694j0j9&sourceid=chrome&ie=UTF-8
- ↑ https://www.childism.org/about