Nenda kwa yaliyomo

Mtumiaji:Kisare/Kalkulasi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kalkulasi ni elimu ya hisabati ya mabadiliko endelevu. Ina matawi mawili makuu: kalkulasi tenguo na kalkulasi kamilisho. Lile la kwanza linahusu viwango vya papohapo na miinamo ya michirizo. Lile la pili linahusu kujumlisha viduchu, na maeneo yaliyoko chini au kati ya michirizo. Matawi haya mawili yanahusiana kwa uhakiki wa msingi wa kalkulasi.

Mwishoni mwa karne ya 17, kalkulasi iliendelezwa na Isaac Newton na Gottfried Leibniz wakijitegemea. Kazi za baadaye, kama vile kupanga kanuni ya mipaka, ziliimarisha nadharia ya Newton na Leibniz. Leo, kalkulasi hutumika sana katika sayansi, uhandisi, na elimujamii.