Mtumiaji:Divine Albert Maguge

    Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

    Nengo

    Nengo ni jina la Mtaa wa mji wa Kibondo, Mkoa wa Kigoma Nchini Tanzania, Mtaa huo uko Mashariki ya Kusini mwa Mji huo. Pia katika mtaa huo, upo mlima wenye jina hilo "Nengo".Anuani ya kijiografia ni -3.607947,30.747422

    Ni moja ya maeneo muhimu katika Wilaya ya Kibondo, kwa kuzalisha aina mbalimbali za nafaka, kama vile Mahindi, Mtama, Maharage, Kunde, karanga, Njegere, Choroko, Mbaazi, nk Huzalisha mazao mengine kama Magimbi, Viazi vikuu, Mihogo, Viazi vitamu, Ndizi nk. Shughuli za uzalishaji wa mazao hayo zimekuwa zikifanyika katika mashamba yaliyoko pembezoni mwa mji huo, kama vile Kumkenga, Kamajeri, Rutende, Katoke, Kakungwe, Kagoti, Ruvunagula, Kagomero, Nyabhihuna, Kisenga, Kumbizi nk.

    Lengo la historia fupi hiyo ni kukutaka ujue ni wapi nilipodondosha kitovu, mengineyo yanapatikana ktk tovuti yangu.