Main (mto)
Mandhari
(Elekezwa kutoka Mto Main)
Main ni mto nchini Ujerumani. Ina urefu wa kilomita 524 ikiwa ni tawimto kubwa la mto Rhine. Uvujaji wake wa wastani katika Bandari ya Frankfurt Mashariki ni mita za ujazo 190 kwa sekunde. Inatiririka kupitia majimbo ya Bavaria, Hesse na kuwa mpaka kati ya Bavaria na Baden-Württemberg.
Jiji kubwa zaidi kwenye Main ni Frankfurt am Main, mengine ni Bayreuth, Bamberg, Würzburg, Hanau na Offenbach[1].
Sehemu ya katikati ya bonde lake kuna mashamba mengi ya mizabibu. Meli ndogo kwenye Main hubeba mizigo kupitia Mfereji wa Rhine-Main-Danubi hadi Ulaya Mashariki na Bahari Nyeusi.[2].
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Main River, Encyclopedia Britannica
- ↑ Corridor 7 ramani ya Pan-European Transport Corridor, tovuti ya United Nations Economic Commission for Europe (UNECE)
Makala hii kuhusu maeneo ya Ujerumani bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Main (mto) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |