Nenda kwa yaliyomo

Frankfurt am Main

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Frankfurt am Main
Frankfurt am Main is located in Ujerumani
Frankfurt am Main
Frankfurt am Main

Mahali pa mji wa Frankfurt am Main katika Ujerumani

Majiranukta: 50°6′37″N 8°40′56″E / 50.11028°N 8.68222°E / 50.11028; 8.68222
Nchi Ujerumani
Jimbo Hesse
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 746.878
Tovuti:  www.frankfurt.de
Soko la Hisa la Frankfurt
Bendera ya Mji wa Frankfurt

Frankfurt am Main ni kati ya miji mikubwa ya Ujerumani. Ina wakazi 747,000. Rundiko la mji wa Frankfurt pamoja na miji mingine kama Mainz na Wiesbaden inaitwa eneo la Rhein-Main lenye wakazi milioni nne.

Frankfurt ni kitovu cha uchumi ch Ujerumani hasa makao makuu ya benki kubwa. Uwanja wa Ndege wa Rhein-Main ni mkubwa katika Ujerumani. Barabara kuu na njia kuu za reli za Ujerumani hukutana hapa.

Frankfurt ni makao makuu ya Benki Kuu ya Ulaya na Benki Kuu ya Ujerumani.

Mji umekuwa na tabia ya kimataifa. Takriban kila mkazi wa tatu ana asili yake nje ya Ujerumani.

Jiografia

[hariri | hariri chanzo]

Frankfurt iko kando la mto Main.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Jina lamaanisha "kivuko cha Wafranki" maana yake mji ulianzishwa kama kijiji cha watu wa kabila la Wafranki pale ambako mto Main ulipitika kwa miguu kwa sababu maji hapakuwa na kina kikubwa. Mpito huu ulisababisha mahali kustawi na kukua.

Frankfurt ikawa mji muhimu wa Dola takatifu la Roma. Makaisari walipokea taji na cheo hapa mjini hadi 1806. Katika karne ya 19 Frankfurt ilikuwa makao makuu ya Shirikisho la Ujerumani. Ilikuwa pia makao ya bunge la kwanza lililochaguliwa kwa uchaguzi huru katika Ujerumani mwaka 1848. Ikakua kuwa kitovu muhimu cha biashara na mawasiliano.

Mji uliharibiwa kabisa wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia na kujengwa upya tangu 1945. Katika Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani tangu 1949 Frankfurt ikawa mji mkuu wa kiuchumi wakati Bonn ilikuwa mji mkuu kisiasa.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu maeneo ya Ujerumani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Frankfurt am Main kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
WikiMedia Commons
WikiMedia Commons