Uwanja wa Ndege wa Rhein-Main
Mandhari

Kiwanja cha Ndege cha Rhein-Main ni kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Frankfurt am Main nchini Ujerumani. Ni kati ya viwanja vya ndege kubwa za abiria zaidi ya milioni 55 wanaopita.[1] Jina kamili kwa Kijerumani ni Flughafen Frankfurt am Main, kwa Kiingereza Frankfurt international Airport. Kifupi chake ni FRA.[2]
Ni kituo kikuu cha Lufthansa.
Kiwanja cha ndege kipo kilomita 12 kusini ya Frankfurt na safari kwa treni kutoka mjini ni dakika 20.
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Frankfurt Airport (FRA)". International Airport Review (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2025-07-10.
- ↑ "Frankfurt Airport - Facts and Figures at FRA". www.frankfurt-airport.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-10-01. Iliwekwa mnamo 2025-07-10.
