Nenda kwa yaliyomo

Mtandao wa neva bandia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mtandao wa neva bandia ni kundi la nodi au makutano (kiingereza node) uliohamasishwa na au kuigwa kutoka kwenye mtandao wa neva za ubongo (uliyorahisiswa). Hapa kila duara au nodi inawakilisha neva bandia, na mshale ukiwakilisha mahusiano au muunganiko kutoka mwisho wa neva bandia moja kwenda mwanzo wa neva bandia nyingine.

Mtandao wa neva bandia au mtandao neva bandia (kwa Kiingereza: artificial neural network, kifupi ANN, pia hufupishwa kama neural network, kifupi NN) ni mbinu kwenye taaluma ya akili bandia inayozipa uwezo kompyuta kuchakata taarifa mithili ya ubongo wa binadamu. Ni mbinu ya kujifunza kwa mashine inayojulikana kama kujifunza kwa kina, inayotumia nodi au neva bandia zilizounganishwa kwenye safu ya matabaka yenye muundo unaofanana na ubongo wa binadamu.

Mtandao wa neva bandia unatengeneza mfumo unaojirekebisha (Kiingereza: adaptive system) ambao kompyuta hutumia kijifunza kulingana na makosa na kuendelea kuwa bora zaidi. [1]

Teknolojia nyuma ya mitandao ya neva bandia imehamasishwa na utendaji kazi wa ubongo na mifumo ya neva, mitandao hii inaiga kwa uchache utendaji kazi wa neva za kibiolojia haswa mfumo wa umeme kwenye neva za ubongo.

Neva bandia hupangwa kwenye safu katika namna ambayo mwisho wa kila neva bandia ni mwanzo wa neva bandia nyingine. Muunganiko huu wa neva bandia unaiga mawasiliano kati ya neva za ubongo, kwa njia hii mtandao wa neva bandia hujifunza kwa kurekebisha uzito wa muunganiko baina ya neva bandia. [2]

  1. "What is a Neural Network? - Artificial Neural Network Explained - AWS". Amazon Web Services, Inc. (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2024-01-10.
  2. "Artificial Neural Network - an overview | ScienceDirect Topics". www.sciencedirect.com. Iliwekwa mnamo 2024-01-10.
Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mtandao wa neva bandia kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.