Nenda kwa yaliyomo

Msamalo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Msamalo ni kata ya Wilaya ya Chamwino katika Mkoa wa Dodoma, Tanzania, yenye postikodi namba 41406[1].

Kata hiyo inapatikana Mashariki mwa jiji la Dodoma umbali wa Km 54. Imeundwa na vijiji vitatu ambavyo ni Mgunga, Mlebe na Mnase yalipo makao makuu ya kata. Umbali uliopo kati ya ikulu ya nchi ya Tanzania na makao makuu ya kata ni Km 40 tu.[2]

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 16,413 [3]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 14,142 [4] waishio humo.

Kata hiyo huwa na shule tano za msingi, na wakazi wake wamepata elimu ya msingi kwa asilimia 100!

Wananchi wa Msamalo wengi wao ni Wagogo ambao shughuli zao za kiuchumi ni kilimo na ufugaji: hii imetokana na ukubwa wa maeneo ya wazi ndani ya kata hii. Wananchi hulima kilimo kikubwa cha msimu wa masika na kilimo kidogo cha umwagiliaji baadhi ya maeneo.

Mahindi, mtama, karanga na baadhi ya mazao yenye kuhitaji mvua za msimu hulimwa pia Msamalo. Alizeti ni moja ya zao ambalo hulimwa sana kwa ajili ya mafuta ya mboga na chakula kwa baadhi ya mifugo.

Ng'ombe, mbuzi na kondoo ni kati ya wanyama wanaofugwa na wenyeji wa kata hiyo, pia kuna ndege ambao hufugwa kama vile kuku, khanga n.k.

  1. "Nakala iliyohifadhiwa" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2020-03-21. Iliwekwa mnamo 2017-10-08.
  2. "Gmail". accounts.google.com. Iliwekwa mnamo 2024-12-26.
  3. https://www.nbs.go.tz
  4. "Sensa ya 2012, Dodoma - Chamwino DC" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2016-03-03. Iliwekwa mnamo 2016-05-18.
Kata za Wilaya ya Chamwino - Mkoa wa Dodoma - Tanzania

Buigiri | Chamwino mjini | Chiboli | Chilonwa | Chinugulu | Dabalo | Fufu | Handali | Haneti | Huzi | Idifu | Igandu | Ikombolinga | Ikowa | Iringa Mvumi | Itiso | Loje | Majeleko | Makang'wa | Manchali | Manda | Manzase | Membe | Mlowa Barabarani | Mlowa Bwawani | Mpwayungu | Msamalo | Msanga | Muungano | Mvumi Makulu | Mvumi Misheni | Nghahelezi | Nghambaku | Nhinhi | Segala | Zajilwa


Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Dodoma bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Msamalo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.