Nenda kwa yaliyomo

Mrifaki

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mrifaki (Alfa Persei, Mirfak)[1]
Kundinyota Farisi (Perseus)
Mwangaza unaonekana 1.82
Kundi la spektra F5 I
Paralaksi (mas) 6.43 ± 0.17
Umbali (miakanuru) 510
Mwangaza halisi - –5.1
Masi M☉ 8.5 ±
Nusukipenyo R☉ 68 ±
Jotoridi usoni wa nyota (K) 6,350
Majina mbadala α Persei, 33 Persei, Marfak, Algenib, BD+49 917, CCDM J03243+4951A, FK5 120, GC 4041, HD 20902, HIP 15863, HR 1017, IDS 03171+4930 A, PPM 46127, SAO 38787

Mrifaki (lat. & ing. Mirfak pia α Alfa Persei, kifupi Alfa Per, α Per) ni nyota angavu zaidi katika kundinyota la Farisi (Perseus) na nyota angavu ya 24 kwenye anga la usiku[2].

Mrifaki inayomaanisha “kiwiko” ilijulikana kwa mabaharia Waswahili tangu miaka mingi wakifuata njia yao baharini wakati wa usiku kwa msaada wa nyota. [3]. Walipokea jina hili kutoka Waarabu wanaosema المرفق al-mirfak inayomaanisha „kiwiko" [4]. Kwa matumizi ya kimataifa Umoja wa Kimataifa wa Astronomia ulikubali jina la Kiarabu na kuorodhesha nyota hii kwa jina la "Mirfak" [5] .

Alfa Persei ni jina la Bayer kwa sababu Alfa ni herufi ya kwanza katika alfabeti ya Kigiriki na Mrifaki ni nyota angavu zaidi katika Farisi - Perseus.

Mrifaki iko kwa umbali wa miakanuru takriban 510 kutoka Jua letu na ni mfumo wa nyota mbili. Nyota kuu ni Mrifaki A iliyo na mwangaza unaoonekana wa 1.5 na mwangaza halisi ni -4.8. Spektra yake ni ya aina ya B2. Nyota ya pili B ina mwangaza unaonekana wa 7.5.

Miaka milioni 4.5 – 5 iliyopita Mrifaki ilikuwa nyota angavu kabisa kwenye anga la Dunia. Wakati ule umabli wake na Jua ulikuwa miakanuru 34 pekee na mwangaza wake ulioonekana ulikuwa -3.99.[6]

Kutokana na jotoridi kubwa kwenye uso wake sehemu kubwa ya mng’aro wake unatoka kwenye spektra ya urujuanimno (ultraviolet radiation) na Mrifaki ni chanzo kikubwa cha mnururisho huu angani[7].

  1. vipimo kufuatana na Lyubimkov, Leonid S.; et al. (February 2010)
  2. Perseus - Mirfak – α Persei tovuti ya constellation guide
  3. ling. Knappert 1993
  4. Waarabu walikuwa na jina mbadala الجانب al-janib au „upande“ na hili lilingia pia katia vitabu vya astronomia ya magharibi kama „Algenib“; ilhali hii ni pia jina la Gamma Persei haitumiwi tena sana kwa Perseus, ling. Allen (1899), uk. 331; Waswahili walikuwa pia na jina mbadala „Janabu Farisawi“ yaani „upande wa Farisi (Perseus)“
  5. Naming Stars, tovuti ya Umoja wa Kimataifa wa Astronomia (Ukia), iliangaliwa Novemba 2017
  6. Tomkin, Jocelyn (April 1998)
  7. Wilkinson, E.; Green, J. C.; McLean, R.; Welsh, B. (1996)

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]


  • Allen, Richard Hinckley: Star-Names and their Meanings; kwa G. E. Stechert New York, Leipzig, London, Paris 1899, ukurasa 331 (online kwenye archive.org)
  • Knappert, Jan: The Swahili Names of Stars, Planets and Constellations; The Indian Ocean Review September 1993 Volume 6 No. 3 September 1993, kurasa 6-7, ISSN 1031-2331
  • Lane, Edward William : An Arabic - English Lexicon by in eight parts – 1872 (Perseus Collection Arabic Materials Digitized Text Version v1.1 of reprint Beirut – Lebanon 1968) online hapa
  • Lyubimkov, Leonid S.; et al. (February 2010), "Accurate fundamental parameters for A-, F- and G-type Supergiants in the solar neighbourhood", Monthly Notices of the Royal Astronomical Society, 402 (2): 1369–1379 online hapa