Mohamed Farah

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Mohamed Muktar Jama Farah (alizaliwa Mogadishu, Somalia, 23 Machi 1983 ni mwanariadha kutoka Uingereza. Alishinda medali mbili za dhahabu za Olimpiki mwaka 2012 na 2016. Alishinda mbio za mita 5,000 na 10,000.

Maisha ya Utotoni[hariri | hariri chanzo]

Farah ni pacha na ana kaka. Awali, familia yake ilikuwa katika nchi ya Somalia, mji was Gabiley. Baba yake ni mfanyabiashara na mama yake anakaa nyumbani. Yeye Aliishi nchi ya Djibouti akiwa mtoto. Yeye alikuwa mkimbizi. Yeye Alihamia Uingereza akiwa na miaka 8 na familia yake.

Kama kijana, yeye alifanya kazi katika mgahawa wa McDonalds. Farah alikwenda shule ya sekondari cha Isleworth na Svon. Yeye alikwenda katika chuo kikuu cha Feltham.

Uanariadha[hariri | hariri chanzo]

Yeye alianza kukimbia katika shule ya sekondari. Yeye alifanya mazoezi ya riadha katika chuo kikuu cha St. Mary’s. Ushindi mkubwa wa kwanza wa Farah ulikuwa mwaka wa 2001 katika Ufaransa. 

Katika mwezi wa tano, mwaka wa 2008, Farah alikimbia mbio za mita 10,000, ambazo zilikuwa za kasi haraka zaidi katika Uingereza kwa muda wa karibu miaka minane.

Yeye hakushiriki katika Olimpiki mwaka wa 2008 Katika mji wa Beijing, nchi ya China.

2011 ilikuwa mwaka mzuri kwa Farah. Yeye alishinda medali ya fedha katika michuano ya dunia katika nchi ya Korea ya Kusini.

Katika michezo ya Olimpiki ya London mwaka wa 2012, tarehe 4 mwezi wa nane, Farah alishinda medali ya dhahabu katika mbio za mita 10,000 kwani alikimbia kwa wakati wa 27: 30.42. Hii ilikuwa medali ya dhahabu ya kwanza ya Olimpiki ya Uingereza katika mita 10,000. Tarehe 11, mwezi wa nane, mwaka 2012 yeye pia alishinda medali ya dhahabu katika mita 5000 kwa wakati wa 13: 41.66.

Farah alishinda medali ya dhahabu katika mita 10,000 katika michezo ya Olimpiki ya mji wa Rio, nchi ya Brazil 2016, tarehe 13, mwezi wa nane.Yeye kwa mara ya kwanza aliwezesha Uingereza kushinda medali ya dhahabu ya tatu. Farah aliendelea na kushinda medali ya pili ya dhahabu katika mita 5,000 katika Olimpiki za mji wa Rio, nchi ya Brazil, tarehi 20.

Maisha yake binafsi[hariri | hariri chanzo]

Farah alifunga ndoa na Tania Nell tarehe 1 Aprili 2010 katika nchi ya Uingereza, mji wa London. Yeye ana binti wa kambo ambaye anaitwa Rihanna. Yeye ana watoto pacha wanaoitwa Aisha na Amani. Wao walizaliwa mwezi wa nane, mwaka wa 2012. Pia, yeye ana mwana anayeitwa Hussein. Mwana wake alizaliwa mwaka wa 2015.

Farah sasa anaishi Uingereza pamoja na familia yake. Yeye sasa amestaafu.

Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mohamed Farah kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.