Mnara wa BCEAO (Bamako)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Mnara wa BCEAO ni jengo linalopatikana huko Bamako, Mali. Lina orofa 20 na urefu wa meta 80 (futi 262),[1] ndilo jengo refu zaidi katika eneo la Afrika Magharibi. Linapatikana upande wa kaskazini ("kulia→") wa ukingo wa Mto Niger katikati mwa Jiji la Bamako.

Mnara huo unaainishwa kama usanifu wa kisudani wa kisasa, yani Neo-Sudanic, umeundwa kwa muundo wa kisudani na kisaheli wa misikiti maarufu ya Djenné na Timbuktu. Jengo hilo, lenye rangi ya chungwa iliyokolea, linalingana na usanifu wa jadi wa banco wa Afrika Magharibi, pamoja na ule wa udongo katika eneo jirani. Umbo lake lililochongoka linafanana na kichuguu cha mchwa kutoka kwa mbali. Pembe za kipekee (au "masikio ya popo") kwenye sehemu ya juu ya jengo, na sehemu yake ya mbele iliyochongwa kwa kina, iliyochanwa wima ni mambo ya kawaida ya mapambo ya usanifu wa Kisaheli, yanayopatikana kwenye majengo kama vile Msikiti Mkuu wa Djenné, na lina mfanano mkubwa mno na jengo la Soko la Bamako la 1923.

Mnara wa BCEAO ni makao makuu ya Benki Kuu ya Mataifa ya Afrika Magharibi nchini Mali, ambayo hutoa huduma za benki za kimaendeleo na za serikali za ufadhili na sarafu katika mataifa kadhaa ya Afrika Magharibi yazungumzayo Kifaransa.

Jengo hili liko katika kitongoji cha Commune III chenye shughuli nyingi, ambapo barabara ya Moussa Tavele inakutana na barabara ya kando ya maji kati ya madaraja mawili makuu ya Bamako: daraja la mfalme Fahad baada ya jengo moja magharibi, na daraja la wafiadini baada ya majengo matatu mashariki. Upande wa mashariki wa uwanja wa BCEAO, mbuga na bustani rasmi ambapo "Boulevard du Peuple" hupita kwa mwelekeo wa mshazari mpaka kufika mtoni. Mkabala kwake kuna bustani ndogo za soko na vituo vya kurushia maji na mitumbwi ipo kwenye kingo za mto. Pamoja na Hotel de l'Amitié na Grande Mosquée, Mnara wa BCEAO ni mojawapo ya alama tatu zinazoonekana katika sehemu kubwa ya jiji.

References[hariri | hariri chanzo]

  1. "BCEAO Tower - The Skyscraper Center". www .skyscrapercenter.com. Iliwekwa mnamo Aug 18, 2020.  Check date values in: |accessdate= (help)