Mlango wa Hudson
Mandhari
Mlango wa Hudson unaunganisha Bahari ya Atlantiki na Ghuba ya Hudson huko Kanada. Uko kati ya Kisiwa cha Baffin na pwani ya kaskazini ya Quebec. Urefu wake ni km 720 mile 450 (km 720), upana wake huwa kati ya km 240 hadi km 54. [1] [2]
Njia hii ya bahari iligunduliwa na nahodha Mwingereza Henry Hudson mnamo mwaka wa 1609 alipotafuta mapito ya kaskazini-magharibi yaani njia mbadala ya kufika kwenye Bahari Pasifiki.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Trémaudan, Auguste Henri de Trémaudan (1916). The Hudson Bay road (1498-1915) (toleo la Digitized Jul 10, 2008). J.M. Dent. uk. 50.
- ↑ answers.com