Mkutano wa Mashirika ya Kitaifa ya Makoloni ya Ureno
Mkutano wa Mashirika ya Kizalendo ya Makoloni ya Ureno (kwa Kireno: Conferência das Organizações Nacionalistas das Colónias Portuguesas, kifupi: CONCP) lilikuwa shirika la kuratibu ushirikiano katika harakati za kitaifa za ukombozi wa makoloni ya Ureno barani Afrika wakati wa vita vya kikoloni vya Ureno.
CONCP ilianzishwa tarehe 18 Aprili 1961 huko Casablanca, Moroko na PAIGC ya Guinea-Bissau na Cape Verde, MPLA ya Angola, UDENAMO (baadaye ikawa FRELIMO) ya Msumbiji na MLSTP ya Sao Tome na Principe. [1] Ujumbe wa raia wa India kutoka Goa pia walihudhuria, pamoja na Aquino de Braganca. [2] Marcelino dos Santos wa UDENAMO aliteuliwa kuwa katibu mkuu wa kwanza wa CONCP na Mario Pinto de Andrade wa MPLA kama rais wa kwanza. [3] [4] CONCP ilibadilisha Medani ya Mapinduzi kwa Uhuru wa Kitaifa wa Makoloni ya Ureno (Kireno huitwa: Frente Revolucionaria Africana para a Independencia Nacional das colonias portuguesas FRAIN) ambayo ilianzishwa na PAIGC na MPLA huko Tunis mnamo mwaka 1960. [5] Mkutano wa pili wa CONCP ulifanyika Dar es Salam, Tanzania, mnamo Oktoba mwaka 1965. [6]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Conferência : A CONCP – a internacionalização da luta pela independência das colónias portuguesas : 15 jun. '16 | 14h30 - 18h30". www.bnportugal.gov.pt. Iliwekwa mnamo 2021-07-12.
- ↑ "Conferência : A CONCP – a internacionalização da luta pela independência das colónias portuguesas : 15 jun. '16 | 14h30 - 18h30". www.bnportugal.gov.pt. Iliwekwa mnamo 2021-07-12.
- ↑ "Conference of Nationalist Organizations of the Portuguese Colonies", Wikipedia (kwa Kiingereza), 2021-03-19, iliwekwa mnamo 2021-07-12