Mkataba wa Moroko – Kongo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Mkataba wa Moroko na Kongo ulisainiwa tarehe 4 Novemba 1911 huko Berlin kati ya Ufaransa na Ujerumani kutambua utawala wa Ufaransa juu ya Moroko. Hafla hii ilihitimisha Mgogoro wa Agadir. Ufaransa ilitoa kwa Ujerumani sehemu za Kongo ya Ufaransa na Afrika ya Ikweta ya Ufaransa, ikijumuisha sehemu ya Kamerun.[1]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "KAISER'S SON SHOWS ANGER AT TREATY; Openly Applauds Criticism of German Backdown by Members of Reichstag.", The New York Times (kwa American English), 1911-11-10, ISSN 0362-4331, iliwekwa mnamo 2021-07-18