Mkataba kuhusu anga-nje

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Mkataba kuhusu ya anga-nje (Outer Space Treaty; kwa kirefu: Treaty on Principles Governing the Activities of States in the Exploration and Use of Outer Space) ni mapatano yanayotawala uhusiano kati ya mataifa ya Dunia katika anga-nje.

Mkataba huu ulianzishwa kama mapatano baina Marekani, Umoja wa Kisovyeti na Ufalme wa Maungano (Uingereza) mwaka 1967 na mataifa yote yalikaribishwa kujiunga nao. Hadi Aprili 1967 nchi 107 zilitia sahihi na kukubali kisheria masharti yake.

Shabaha ya mkataba huu ilikuwa maelewano juu ya usalama wa kisiasa kwenye anga-nje.

  1. Fungu na. 1 linatoa ruhusa kwa mataifa yote yanaruhusiwa kuendesha utafiti wa kiraia kwenye anga-nje "Anga-nje, pamoja na Mwezi na magimba mengine ya angani, litakuwa eneo huru kwa upelelezi na matumizi na nchi zote bila ubaguzi wa namna yoyote, kwenye msingi wa usawa na kwa kupatana na sheria ya kimataifa, na kutakuwa na fursa ya kuingia katika maeneo yote ya magimba ya angani"[1]
  2. Fungu na. II linakataza kutwaliwa kwa magimba ya anga (kama Mwezi) na taifa lolote; wakati ule ililenga hasa kuzuia nchi yoyote kuleta madai eti Mwezi ni mali yao.
  3. Fungu na. IV linakataza silaha za nyuklia na silaha nyingine za maangamizi ya watu wengi kupelekwa angani; hairuhusiwi kuanzisha vituo vya kijeshi kwenye anga-nje au kwenye magimba ya anga
  4. Fungu na. VII linaeleza ya kwamba kila nchi inawajibika kwa hasara kutokana na shughuli zake katika anga-nje (kwa mfano kuanguka kwa satelaiti au roketi kwa makazi ya watu mahali popote duniani)[2]

Katika Afrika ya Mashariki Uganda (tangu 1968) na Kenya (1984) ni washiriki kamili wa mkataba huu; serikali za Rwanda na Burundi zilitia sahihi kwenye mwaka 1967 lakini bila kutafuta idhini ya mabunge yao.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya sheria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkataba kuhusu anga-nje kama historia yake au uhusiano wake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.