Nenda kwa yaliyomo

Miroslav Bulešić

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Miroslav Bulešić

Miroslav Bulešić (alizaliwa 13 Mei 192024 Agosti 1947) alikuwa kasisi wa Kanisa Katoliki la Kirumi kutoka Kroatia. Alisoma huko Roma kabla ya kurejeshwa kwao Istria, eneo lake la asili, ambako alipewa daraja ya upadrisho mwaka 1943 wakati wa Vita vya Pili vya Dunia. Baada ya kutumikia katika parokia mbili, alijulikana kwa kuwa mkosoaji mkubwa wa Ukomunisti. Alifufua maisha ya kiroho katika parokia alizohudumu kupitia shughuli za kichungaji zilizopangwa vizuri na alihimiza waumini kushiriki mara kwa mara katika sakramenti. Hata hivyo, ukosoaji wake dhidi ya Ukomunisti ulimletea maadui waliomshambulia na kufanikiwa kumuua.

Alitangazwa mwenye heri nchini Kroatia tarehe 28 Septemba 2013 baada ya kutambuliwa kuwa aliuawa "in odium fidei" ("kwa chuki dhidi ya imani"). Sherehe ya kumtangaza iliongozwa na Kardinali Angelo Amato kwa niaba ya Papa Fransisko.[1]

Kaburi kutoka 1958 hadi 2003.
  1. "Blessed Miroslav Bulešić". Saints SQPN. 18 Juni 2016. Iliwekwa mnamo 2 Juni 2016.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.