Nenda kwa yaliyomo

Michael Vaughn

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Michael Vaughn
muhusika wa Alias

Michael Vaughn, kacheza kama Michael Vartan
Mwonekano wa kwanza "Truth Be Told"
(sehemu ya 1.01)
Mwonekano wa mwisho "All the Time in the World"
(sehemu ya 5.17)
Imechezwa na Michael Vartan
Maelezo
Majina ya utani Vaughn
Majina mengine André Micheaux
(jina la kuzaliwa)
BoyScout (msimu wa 1-3)
Shotgun (msimu wa 4-5)
Jinsia Kiume
Kazi yake Kachero ugani wa CIA
Kachero ugani waAPO
Ndoa Lauren Reed
(mke; amekufa)
Sydney Bristow
(mke)
Watoto Isabelle Vaughn
(binti,amezaa na Sydney)
Jack Vaughn
(mtoto, amezaa na Sydney)
Ndugu William Vaughn
(baba; amefariki)
Jack Bristow
(baba-mkwe; amefariki)
Irina Derevko
(mama-mkwe; amefariki)
Nadia Santos
(shemeji; amefariki)
Utaifa Mmarekani

Michael C. Vaughn ni jina la kutaja uhusika wa kwenye mfululizo wa kipindi cha televisheni cha Alias. Uhusika umechezwa na Michael Vartan, Vaughn ni mmoja kati ya wafanya-wenzi wa Sydney Bristow na vilevile ndiye kipenzi chake cha baadaye na kuendelea. Yeye, kama Sydney, ana maarifa katika nyanja mbalimbali. Vipawa vyake vya kilugha, vinaonekana katika sehemu mbalimbali, ikiwa ni pamoja na Kifaransa, Kihispania, Kiitalia, na nyingine nyingi tu.

Kupitia katika misimu mitatu ya mwanzo, jina msimbo lake lilikuwa BoyScout; kuanzia msimu wa nne na kuendelea, lilikuwa Shotgun. Kwenye msimu wa tano, jina la kuzaliwa la Vaughn lilijulikana kuwa ni André Micheaux.

Wasifu na uhusika

[hariri | hariri chanzo]

Michael Vaughn awali alikuwa msimamizi wa Sydney Bristow wakati anafanya kazi kama kachero-maradufu wa CIA ndani ya SD-6. Lakini polepole, makachero hao wawili wakaanza kutengeneza hisia za kimahaba na wawili hao walifanya kazi kwa karibu kuhakikisha kwamba wamelitokomeza shirika la kijasusi. Hili limepelekea kumfurahisha baba wa Sydney, Jack Bristow, kachero-maradufu mwingine ndani ya SD-6.

Mahusiano ya Vaughn na Sydney yamekuwa wazi baada ya kuangamizwa kwa SD-6 wakati wa msimu wa pili. Pale Sydney alipouawa dhahiri kwenye moto miezi michache baadaye, Vaughn aliyevunjika moyo ameacha kazi CIA na kupata kazi kama mwalimu wa lugha ya Kifaransa. Pia alipata kujihusisha na mfanyakazi wa NSC Bi. Lauren Reed na kisha baadaye kumuoa wakati fulani-kipindi cha miaka miwili ya kupotea kwa Sydney.

Pindi alipogundua kwamba Sydney bado yu hai, Vaughn akarudi CIA na kwa haraka zaidi akaona hisia zake sio imara kwa mkewe, kiukweli kwamba ilileta shida na wasiwasi mkubwa kwa ndoa ya Lauren. Hatimaye, ikagundulika kwamba Lauren alikuwa kachero-maradufu wa Kina Covenant na kwamba Lauren amemtongoza Michael ili apate habari juu ya Sydney. Vaughn akawa na huzuni na kukamatwa kwa Sydney na akatiwa moyo na Jack Bristow kumuua Lauren, ambapo alifanya mwishoni mwa msimu wa tatu. Kitendo hicho kiliendelea kumzuru katika sehemu ya msimu wa nne japokuwa amempiga risasi Lauren ili kumkinga asimuue Sydney.