Mgomo mkuu wa Nigeria wa mwaka 1945
Mgomo mkuu wa Nigeria wa mwaka 1945 ulifanyika katikati ya mwaka na ulikuwa wa kwanza na wa aina yake kutokea katika taifa, ukikusanya wastani wa wafanyakazi 200,000 na vyama vya wafanyakazi kumi na saba.
Historia
[hariri | hariri chanzo]Kuanzia mwaka 1914 hadi 1960 Uingereza ilishikilia Nigeria kama koloni.[1] Wakati wa Vita vya pili vya Dunia, ambapo koloni hilo lilishiriki, [2] Nigeria kulikuwa na mfumko mkubwa wa bei pamoja na ongezeko la mishahara uliodorora. katika kuchangia juhudi za vita Watu wa nigeria wengi walijikuta wakifanya kazi zaidi.[2] [3] Jaribio la serikali kudhibiti bei lilikuwa limeonekana kushindikana.[2]
Muungano wa wafanyakazi ulidai mshahara wa kiwango cha chini mnamo 22 Machi 1945, ambayo serikali ilikataa kutoa 2 Mei. Mwitikio wa wafanyakazi ni kwamba walitoa taarifa kuwa serikali imekataa kutoa mahitaji yao siku ya "Alhamisi, Juni 21, 1945, wafanyakazi wa Nigeria waliendelea kutafuta suluhisho lao kwa kuzingatia sheria na utaratibu kwa upande mmoja na upande mwingine”. Mkutano kati ya serikali na viongozi wa wafanyakazi mnamo Mei 30 haukusuluhisha matatizo yao. Katika kujaribu kutuliza wafanyakazi, mnamo Juni 2 serikali ilimwachilia Michael Imoudu, kiongozi mashuhuri wa wafanyakazi ambaye alikuwa gerezani tangu mwaka 1943, na wiki iliyofuata ilihidhinisha ongezeko dogo la mshahara ambalo wagomaji walilikataa. Badala ya kutolewa kwa Imodu kuliwatia moyo na kumfanya kuwa kiongozi wa mgomo. Hakuna makubaliano yoyote yaliyoafikiwa, na wafanyakazi walikuwa tayari kugoma.[2] [3]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Nigeria | History, Population, Flag, Map, Languages, Capital, & Facts". Encyclopedia Britannica (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2021-08-24.
- ↑ 2.0 2.1 2.2 2.3 Oyemakinde, Wale (1975). "THE NIGERIAN GENERAL STRIKE OF 1945". Journal of the Historical Society of Nigeria. 7 (4): 693–710. ISSN 0018-2540.
- ↑ 3.0 3.1 "Can Nigeria repeat the 1945 general strike?". The Guardian Nigeria News - Nigeria and World News (kwa American English). 2018-02-12. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-08-28. Iliwekwa mnamo 2021-08-24.