Mfalme Yekonia
Mandhari
Mfalme Yekonia (kwa Kiebrania יְכָנְיָה, Yekonia, au יְהֹויָכִין, Yehoiakin, pia kifupi Konia) alikuwa mtawala wa ufalme wa Yuda kutoka ukoo wa Daudi.
Alitawala miezi mitatu tu (9 Desemba 598 KK - 15 Machi 597 KK) baada ya baba yake mfalme Yehoyakimu huku mji wa Yerusalemu ukiwa umezingirwa na jeshi la mfalme Nebukadneza II kutoka Babuloni.
Mji ulipotekwa, aliondolewa madarakani (2Fal 24:17) na kupelekwa uhamishoni alipokaa gerezani miaka 37.
Hatimaye alitolewa na kuwa mgeni wa mfalme wa Babuloni hadi kifo chake (2Fal 25:27): habari hiyo imeandikwa mwishoni mwa kitabu cha pili cha Wafalme kama utangulizi wa ukombozi wa Wayahudi wote.
Kama alivyotabiri nabii Yeremia (Yer 22:28-30), hakuna mzao wake aliyetawala tena.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Jehoiachin in Babylonia Archived 2 Februari 2011 at the Wayback Machine., discussion of the Babylonian evidence
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mfalme Yekonia kama habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |