Nenda kwa yaliyomo

Yehoyakimu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Mfalme Yehoyakimu)
Mfalme Yehoyakimu alivyochorwa na Guillaume Rouillé katika Promptuarii Iconum Insigniorum mwaka 1553.

Yehoyakimu (kwa Kiebrania יְהוֹיָקִים, Yehoyakim, "Yule ambaye YHWH amemuinua") (635 KK - 597 KK) alikuwa mtu wa ukoo wa Daudi aliyetawala ufalme wa Yuda kwa miaka 11 (608 KK hadi kifo chake)[1] baada ya mdogo wake Shallumu.

Mwana wa pili (1Nya 3:15) wa mfalme Yosia, kabla hajatawazwa na Farao Neko II wa Misri,[2] aliitwa Eliakimu (אֶלְיָקִים, Eliakim).

Alikataa kufuata maelekezo ya nabii Yeremia hata akathubutu kuchana na kuchoma maandishi aliyotumiwa naye (Yer 36:1-32). Zaidi tena, alimuua nabii Uria kwa kutoa ujumbe wa namna hiyohiyo kutoka kwa Mungu (Yer 26:20-23)[3].

Alifariki huku mji wa Yerusalemu umezingirwa na jeshi la Nebukadneza II wa Babuloni. Badala yake alitawazwa mwanae Yekonia.

  1. Dan Cohn-Sherbok, The Hebrew Bible, Continuum International, 1996, page x. ISBN 0-304-33703-X
  2. Oded Lipschits (2002). ""Jehoiakim Slept with his Fathers…" (II Kings 24:6) – Did He?" (PDF). fontes.lstc.edu. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2018-06-02. Iliwekwa mnamo 2018-12-08.
  3. James Maxwell Miller, John Haralson Hayes, A History of Ancient Israel and Judah (Westminster John Knox Press, 1986) page 404–405.
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Yehoyakimu kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.