Masista wa Imakulata wa Mt. Klara

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Masista wa Imakulata wa Mt. Klara ni shirika la kitawa lenye hadhi ya Kipapa ambalo linaendeleza kazi ya malezi iliyoanzishwa mwaka 1741 na akina dada watatu huko Fiuggi (Italia).

Majina ya hao Akina Dada Faioli ni Teresa, Cecilia e Antonia, ambao, kisha kufiwa mama yao wakiwa bado wadogo, hawakukata tamaa, bali kwa kusaidiana walifikia pamoja uamuzi wa kutawa ili kumlenga zaidi Mungu.

Kumbe wasichana wengi wa mji wao walivutiwa na mfano wao wakawatafuta na kupokewa vizuri kwa malezi.

Hiyo “shule iliyoanza toka chini”, kwa kutegemea karama ya wanawake na kulenga ukombozi wao, inakumbusha kwamba vizazi vipya vinahitaji walezi wa kuaminika ambao wawaelekeze tunu za kiadili ambazo ziwaongoze maishani kukomaa na kujenga jamii yenye haki, amani na upendo.

Kwa sasa masista hao wako katika jumuia nyingi za Italia, lakini pia Brazil, Ufilipino na Tanzania.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Tovuti rasmi ya shirika kwa lugha nne, mojawapo ikiwa Kiswahili Archived 26 Machi 2009 at the Wayback Machine.