Masi ya Jua

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ulinganifu wa masi za nyota: nyota kibete nyekundu (M 0.1), Jua, nyota kibete buluu (M 8) na R136a (M 300)

Masi ya Jua (ing. Solar mass) inataja masi ya Jua letu ambayo ni takriban kilogramu 1.99 × 1030 . Hii inalingana na masi ya Dunia yetu mara 332,946.

Kiwango hiki hutumiwa kama kizio katika sayansi ya astronomia kwa kutaja masi ya magimba kwenye anga ya nje hasa nyota, fungunyota na galaksi.

Nyota nyingi huwa na masi baina ya x0.1 na x10 ya masi ya Jua. Mara chache kuna nyota kubwa sana yenye masi x250 za Jua. Hivyo Jua letu liko kwenye wastani wa masi za nyota kati ya nyota za safu kuu.

Ilhali masi ya Jua inaendelea kupungua polepole kutokana na mnururisho na upepo wa Jua kuna ufafanuzi wa Umoja wa Kimataifa wa Astronomia wa kuhesabu masi ya Jua kuwa kilogramu 1.9891×1030[1].

Alama yake ni M ambako "M" inamaanisha "masi" na ☉ ni ishara ya Jua.

Vizio vinavyolingana

Masi moja ya Jua inalingana na

  • 27,068,510 x masi ya Mwezi M
  • 332,946 x masi ya Dunia M
  • 1,048 x masi ya Mshtarii M.

Njia Nyeupe (galaksi yetu) ina takriban milioni 180 masi za Jua ambayo inalingana na kilogramu 3.6 · 1041.


Marejeo

  1. Measuring the Universe - The IAU and astronomical units, tovuti ya Ukia, iliangaliwa Novemba 2017
Astrowiki.PNG
Mradi wa Astronomia Makala hii imewahi kukaguliwa na kuboreshwa kwenye warsha ya pamoja ya Jenga Wikipedia ya Kiswahili, Wikimedia Community User Group Tanzania na ASSAT. Imepewa hali ya ulinzi. Tunaomba mapendekezo yote ya usahihisho na nyongeza zipelekwe kwanza kwenye ukurasa wa majadiliano