Martin Linnes

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Martin Linnes (alizaliwa 20 Septemba 1991) ni mchezaji wa soka wa Norway ambaye anacheza kama beki wa kulia katika klabu ya Uturuki ya Galatasaray. Ni mchezaji hodari, pia alishawahi kucheza kama beki wa kushoto, kiungo wa kati, kiungo wa kulia.

Kazi ya kilabu[hariri | hariri chanzo]

Miaka ya mapema[hariri | hariri chanzo]

Linnes alianza kazi yake huko Sander, kisha akajiunga na Kongsvinger. Mnamo mwaka wa 2010, alifcheza kwa mara ya kwanza katika klabu hiyo.

Molde[hariri | hariri chanzo]

Linnes alijiunga na klabu ya Molde mnamo mwaka 2012, baada ya mkataba wake na klabu ya Kongsvinger kumalizika katika msimu wa 2011-12.

Mnamo 9 Aprili 2012, alicheza mchezo wake wa kwanza dhidi ya klabu ya Brann, ambayo Molde walishinda 2-1, na mnamo 4 Agosti 2012, alifunga goli lake la kwanza dhidi ya klabu ya Sogndal, katika mechi ambayo Molde alishinda 2-1.

Tarehe 17 Septemba 2015, Linnes alifunga goli la tatu dhidi ya Fenerbahçe katika hatua ya makundi msimu wa 2015-16 katika mashindano ya UEFA Europa League.

Baada ya miaka 4 akiwa na klabu ya Molde, Linnes alikubaliana na Galatasaray ,na alicheza michezo 152, akifunga magoli 14 na kutoa pasi za mwisho zilizosaidia magoli 26 akiwa na klabu ya Molde.

Galatasaray[hariri | hariri chanzo]

Mnamo Januari 2016, Linnes alisaini mkataba wa miaka 3½ na klabu ya Uturuki ya Galatasaray kwa ada ya uhamisho wa milioni 2. Alichukua jezi namba 27 iliyowahi kuvaliwa na mchezaji wa zamani, Emmanuel Eboué. Alichezaa kwa mara ya kwanza dhidi ya Akhisar Belediyespor kwenye Kombe la Uturuki msimu wa 2015-16, mechi iliyomalizika kwa sare ya 1-1.

Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Martin Linnes kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.