Martin Ødegaard

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Martin Ødegaard

Martin Ødegaard (alizaliwa 17 Desember 1998 )[1] [2] [3] ni mchezaji wa mpira wa miguu ambaye anacheza kama kiungo mshambuliaji katika klabu ya mpira wa miguu ya Arsenal[4] na nahodha wa timu ya taifa ya Norway.

Ødegaard alianza kazi ya mpira kwenye vilabu vikubwa akiwa na umri wa miaka 15 mnamo 2014 akichezea Strømsgodset.Aliweka rekodi ya mfungaji bora mwenye umri mdogo , na mnamo 2015 alijiunga na Real Madrid kwa uhamisho wa thamani ya €4 milioni, ambapo aliweka rekodi ya kuwa mchezaj mwenye umri mdogo.

Ødegaard alicheza mechi yake ya kwanza ya kimataifa akitumikia Norway mwaka wa 2014, akiwa na umri wa miaka 15, na ameweka rekodi ya kuwa mchezaji mwenye umri mdogo zaidi wa timu ya taifa ya Norway, na mchezaji mwenye umri mdogo zaidi kucheza mechi ya kufuzu kwa UEFA Europa.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Martin Ødegaard: Overview. ESPN.
  2. Acta del Partido celebrado el 23 de mayo de 2015, en Madrid (es). Royal Spanish Football Federation. Jalada kutoka ya awali juu ya 2023-04-17. Iliwekwa mnamo 2022-05-23.
  3. Martin Ødegaard: Overview. Premier League.
  4. Teen star Odegaard headlines Norway squad to face Socceroos. Special Broadcasting Service.
Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Martin Ødegaard kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.