Mark Ruffalo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Mark Alan Ruffalo (/ˈrʌfəloʊ/; amezaliwa Kenosha, Wisconsin, Novemba 22, 1967) ni muigizaji na mtayarishaji wa filamu wa Marekani.

Alianza kuigiza mnamo miaka ya 1990 na kupata umaarufu mkubwa kutoka kwenye maigizo mbalimbali kama vile This is our youth na You Can Count On Me. Aliendelea na maigizo na akajulikana zaidi pale alipokua mhusika katika filamu zilizotengenezwa na Marvel Studios kama Bruce Barner (Hulk) ambapo aliigiza filamu kama vile The Avengers (2012), Avengers: Age of Ultron (2015), Thor: Ragnarok (2017), Avengers: Infinity War (2018), na Avengers: Endgame (2019).

Maisha ya awali[hariri | hariri chanzo]

Mama yake aitwaye Marie Rose alikuwa msusi wa nywele na baba yake Frank Lawrence Ruffalo Jr, alikuwa mpaka rangi katika majengo. Ana dada wawili ambao ni Tania na Nicole, pia alikuwa na kaka aliyeitwa Scott ambaye alifariki mwaka 2008.

Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mark Ruffalo kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.