Marioo
Marioo (jina lake halisi ni Omary Mwanga; alizaliwa Temeke, Dar es Salaam, Tanzania) ni mwimbaji wa Bongo Flava, pia mtunzi na mtayarishaji wa nyimbo. [1]
Baada ya kuzaliwa jijini, alipelekwa kijijini kwa bibi yake Kibiti, mkoa wa Pwani, na huko ndiko alikokulia, kwa kuwa yeye anatokea katika kabila la Wandengereko.
Marioo alianza safari yake ya muziki kama mtunzi wa nyimbo akitunga nyimbo kama "Wasikudanganye" iliyoimbwa na mwanamuziki wa Tanzania anayeitwa Nandy ¨The African Princess¨.
Pia aliandika wimbo wa "Unaniweza" ulioimbwa na Jux na ni mmiliki wa hit song "beer tam" iliyoshinda tuzo za TMA kama wimbo bora wa mwaka 2021/2022.
Wimbo wake wa kwanza ni "Dar Kugumu" mwaka 2017. Kabla ya kuendelea kutengeneza jina lake kwa kutoa nyimbo nyingine kama Inatosha, Unanionea, AYA, Raha, Chibonge, Mama Aminah, Hakuna Matata na Beer Tamu.
Pia amefanikiwa kufanya kolabo na wasanii wa nchi mbalimbali ikiwemo Afrika Kusini.
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Tanzania bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Marioo kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |