Jux

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Juma Mussa (anajulikana kwa jina la kisanii Jux; amezaliwa 1 Septemba, 1989) ni mwimbaji wa muziki wa kizazi kipya kutoka nchini Tanzania. Ana asili mchanganyiko kutoka Mikoa ya Mtwara na Morogoro.

Jux alianza kuvuma kwa nyimbo zake za Nimedata, Mwambie, Uzuri Wako, Nitasubiri, Sisikii, Juu na Utaniua.

Jux ni msanii wa R&B aliyefanya video zake nyingi nchi za nje kushinda wasanii wengi wa R&B nchini Tanzania.

Aliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Vanessa Mdee uliodumu kwa miaka takribani 7.[1]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Musical notes.svg Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Jux kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.