Nenda kwa yaliyomo

Mario Brega

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mario Brega kama mlinzi wa wafungwa "Wallace" katika filamu ya the Good, the Bad and the Ugly.

Mario Brega (Roma, 5 Machi 1923 - Roma, 23 Julai 1994) alikuwa mwigizaji wa Italia. Brega, kiumbo alionekana kuwa na mwili mkubwa, kitu ambacho kinaashilia kuwa yeye ni jambazi, kama ilivyokuwa katika filamu zake za awali za kutoka western.

Brega akisimama alivuka urefu wa futi sita, japokuwa vipimo vyake vimebaki kuwa havieleweki, ila tu, unaweza kuchukulia urefu wake kuwa unafanana na ule wa Clint Eastwood wa miaka ya 1960.

Maisha ya Mwanzo[hariri | hariri chanzo]

Brega alizaliwa mjini Rome, Italia. Mwanzoni alikuwa anafanya kazi machinjioni, kabla ya kujiingiza katika masuala ya uigizaji. Umbo lake kubwa lilimthibitishia kuwa yeye ana uwezo wa kucheza filamu sehemu za hatari.

Mwanzoni alicheza filamu sehemu ndogo, hasa katika filamu zilizokuwa zinaongozwa na "Dino Risi", kisha akaja kucheza tena katika baadhi ya filamu ziliongozwa na Sergio Leone, maarufu kama Spaghetti Western, ikiwemo, A Fistful of Dollars, alicheza k.m Chico, For a Few Dollars More, alicheza k.m Nino, The Good, the Bad and the Ugly, alicheza k.m Wallace, na pia akacheza kama mjambazi katika Once Upon a Time in America.

Brega pia alionekana katika filamu nyingine nyingi tu za spaghetti Westerns, ikiwemo Death Rides a Horse, The Great Silence, na My Name is Nobody. Brega pia alishiriki katika baadhi ya filamu za muongozaji Federico Fellini, kisha baadae akawa anashughulisha na filamu za vichekesho, akiwa sambamba na muongozaji Carlo Verdone.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mario Brega kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.