Mario Been

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Mario Been
Mario Been (2007).jpg
Maelezo binafsi
Jina kamili Mario Been
Tarehe ya kuzaliwa 11 Desemba 1963
Mahala pa kuzaliwa    Rotterdam, Oholanzi
Nafasi anayochezea Katikati
Maelezo ya klabu
Klabu ya sasa Staafu

* Magoli alioshinda

Mario Been (amezaliwa Rotterdam, Zuid-Holland, 11 Desemba 1963) ni kocha wa mpira wa miguu kutoka nchini Uholanzi, ambaye ndiye kocha wa klabu ya NEC Nijmegen tangu msimu wa mwaka 2006, alisaidia kurejea kwa klabu ya Excelsior Rotterdam kutoka katika ligi ya pili kuipandisha katika ligi kuu ya Uholanzi. Alipewa lakabu huko Uholanzi la Diego Maradona baada ya jina lake la kwanza.

Yeye kama mchezaji wa mpira wa katikati, Been alizichezea klabu za Feyenoord Rotterdam, Pisa Calcio, Roda JC, Sc Heerenveen, FC Tirol Innsbruck, na Excelsior Rotterdam. Na aliichezea Timu ya Taifa ya Uholanzi kwa mechi moja. Been alicheza mechi yake ya mwisho tarehe 17 Septemba 1995 pindi HFC Haarlem iliifunga Excelsior (4-0).