Maria Sarungi Tsehai

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Maria Sarungi Tsehai

Nchi Tanzania
Kazi yake
  • Mjasiriamali
[1]
Tovuti mariasarungitsehai.wordpress.com


Maria Sarungi Tsehai ni mwanaharakati anayepambana kuwashawishi watu katika nchi ya Tanzania, kukubali kuwa na mabadiliko chanya kupitia kampeni yake katika mitandao ya jamii iitwayo "Change Tanzania”. Change Tanzania ilianza kama hashTag kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter(#changeTanzania)[2] .

Anafahamika pia kwa jinsi anavyoshiriki katika kuwasaidia binti/mabinti wadogo kuzifikia ndoto zao za kuwa gwiji/magwiji wa urembo, kwa kuitumia nafasi yake kama Mkurugenzi wa Miss Universe Tanzania kufundisha na kutoa kipaumbele kwa mabinti hawa. [3][4] .[5]

Elimu[hariri | hariri chanzo]

Maria Sarungi Tsehai ana shahada ya kitivo cha sayansi ya jamii kutoka katika chuo kikuu cha Eötvös Loránd in Hungary, alihitimu mwaka 1999.[6]

Kazi[hariri | hariri chanzo]

Ni mtaalam wa mawasiliano, uandishi wa habari na mambo ya urembo, anamiliki kampuni ya mawasiliano ,compass communication [7] Na yeye ndiye Mkurugenzi katika kampuni hii. Akiwa mkurugenzi ,ameweza kushiriki katika utengenezaji wa filamu ya “Am Tired” ambayo ilifanyika mwaka 2005 na nyingine iitwayo “Born on fire” ya mwaka 2008. .[6]

Harakati[hariri | hariri chanzo]

Sarungi anafahamika sana kwa mawazo yake juu ya namna raia wa nchi ya Tanzania wanaweza kuleta mabadiliko chanya [8]kupitia vyombo vya habari

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Maria Sarungi Tsehai kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.