Maria (Kipindi cha televisheni)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Maria ni kipindi cha televisheni nchini Kenya ya hadithi ya mapenzi iliyoelekezwa na Julian S. Mwanzele inayomshirikisha Yasmin Said kama mwigizaji mkuu,[1] pamoja na Brian Ogana na Bridget Shighadi katika kipindi chao cha kwanza kwenye televisheni. Kilionyeshwa kwa mara ya kwanza Oktoba 10, 2019 na onyesho la mwisho likafanyika Machi 18, 2021, baada ya jumla ya maonyesho 374.[2] Kipindi hiki kilionyeshwa katika runinga ya Citizen TV kila siku ya wiki saa 7:30 usiku saa za Afrika Mashariki na pia katika chaneli ya Viusasa. Kipindi hiki ni kipindi kinachopendwa sana nchini Kenya.

Hadithi hii ya mapenzi inaangazia wahusika watatu wakuu kwenye kipindi— Maria, binti wa kupanga mwenye mvuto; Luwi, kifungua mimba wa aila kwasi ya Hausa na Sofia, mkewe Luwi ambaye lengo lake ni kupokonya mali ya familia ya wakwe zake.

Muhtasari[hariri | hariri chanzo]

Tamthiliya hii inaangazia maisha ya mhusika mkuu Maria (Yasmin Said) pamoja na yanayomkuta jijini Nairobi. Hakuweza kuwaona wazazi wake wa kumzaa, wote ambao waliaga dunia yeye akiwa angali mchanga, hivyo basi, akalelewa na mama mlezi Naomi ambaye pia akaaga dunia baadaye. Maria anakuja kuwa binti wa kupanga kwenye familia ya William Hausa, tajiri mmoja aliyejuana na babake tangu zamani. Kule, anamkuta Luwi ambaye licha ya uanandoa wake na Sofia, anapatwa na hisia za mapenzi juu ya Maria. Maria pia baadaye anagundua kwamba anazo hisia zizo hizo kwa Luwi, na wote wawili nanakuja kuwa wapenzi,. Matukio mengi yanafanyika kama vile Sofia kuigiza uchizi kwa minajili ya kufanikisha mpango wake. Anapojifanya kuwa sawa hatimaye, anaomba talaka yake, jambo linalompa Luwi uhuru wa kumchumbia Maria. Huba hilo lenye kina kirefu linayeyuka ghafla, pindi tu Maria anapogundua kuwa William Hausa ndiye muuaji wa babake na mali zote anazo ni za babake, yakiwemo maovu mengine, yote ambayo aliyasitiri moyoni mwake na hakumruhusu yeyote ayajue. Vile vile, inagundulika kuwa Victor siye mwanawe mzee William wa kumzaa, ya kwamba yeye ni ndugu wa kambo wa Sofia pamoja na Luwi. Anaifurusha aila yake nyumbani kwao na kisha baadaye kuchizika. Mzee William, pamoja na mshauri wake Mejja wanakula njama ya kumfanya Sandra atiwe mbaroni. Sandra, ambaye daima alizama kwenye mapenzi na William asisikie lolote wala chochote, anaahidi kulipiza kisasi baada ya usaliti alioshuhudia. Mzee William anashuhudia ajali mbaya inayomfanya kiwete abadi. Kumwona katika hali hiyo, Maria, aliyekuwa na mpango wa kumfungulia mashtaka William, anamhurumia na kuufutilia mbali wazo hilo la awali. Anaukubali uchumba wa Luwi kwa mara nyingine tena kisha wao wawili wanapanga harusi yao. Kwa bahati mbaya, Sofia anapigwa risasi siku hiyo ya harusi na Brenda ambaye lengo lake lilikuwa ni Maria. Silas anamchumbia Vanessa huku Maggie akihuzunika kwa sababu hata yeye anazo hisia za mapenzi juu yake Silas. Mzee William pia anakamatwa na askari siku hiyo kwa makosa mengi aliyoyafanya hapo nyumaye. Anaaukubali agizo hilo kiurahisi. Miezi michache imepita na waarusi wale wanatarajia kupata mtoto wao wa kwanza. Tunawaona Luwi na Maria wakiifurahia fungate yao na kutembelea mbuga ya wanyama. Wote wanasemezana mapenzi yao huku wakitarajia maisha mema baadaye.

Suala la mapenzi katika Maria[hariri | hariri chanzo]

Luwi anampenda Maria

Silas anampenda Vanessa

Victor anampenda Sonia

Victor anampenda Delilah

Wahusika na waigizaji[hariri | hariri chanzo]

Nakala:[3][4][5]

Waigizaji wakuu[hariri | hariri chanzo]

  • Yasmin Said kama Maria Tino
  • Bridget Shighadi kama Sofia
  • Brian Martins Ogana kama Luwi Hausa
  • Ronald Ndubi kama Victor
  • Dennis Musyoka kama Boss William Hausa
  • Sheila Ndanu kama Madam Victoria Hausa (au Vickie)
  • Wanjiku Stephens kama Vanessa Hausa

Waigizaji wasaidizi[hariri | hariri chanzo]

  • Linda Alexette kama Tobi
  • Teddy Brown kama Fali
  • Belinda Joana kama Kobi
  • Aisha Hussein kama Gloria
  • Umar Hussein kama Pupa
  • Abdalla Ali kama Jayden
  • Botul Abdalla kama Marianne
  • Beatrice Dorea kama Maggie
  • Blessing Lung'aho kama Meja
  • Carol Kipsuto kama Sandra
  • Periz Wambui kama Salome
  • Terry Ombaka kama Naomi
  • Robert Budi kama Trevor
  • Grace Obuya kama Sister Teresa
  • Tina Njambi kama Lorna
  • Christopher Kamau kama Daniel
  • Maureen Wangare kama Brenda
  • Edna Nguka kama Delilah
  • Musa Ore kama Father Ezekiel
  • Nyakundi Isaboke kama Silas
  • Timothy Musyoka kama Ben
  • Tindo Mwanzele kama Mwambe
  • Suzie Malaki kama Rufina
  • Quincy Ando kama Thomas
  • Edwin Buni kama Koros
  • Sarah Malaki kama Mama Chapo
  • Alice Mari kama Kanini
  • Jane Mulanda kama Dogo
  • Joseph Kiplabatt kama Collo
  • Anthony Ashioya kama Tekno
  • Brian Kibochi kama Bondi

Mwigizaji mgeni[hariri | hariri chanzo]

  • Aseem Sharma kama Sonia

Mapokezi[hariri | hariri chanzo]

Nakala:[6]

Kipindi cha kwanza Kipindi cha mwisho Wastani
Tarehe Tathmini Tarehe Tathmini
Oktoba 10, 2019 31.8% Machi 18, 2021 36.8% 29%

Marudio[hariri | hariri chanzo]

Vipindi vyote vya siku za wiki zilirudiwa kila Jumamosi saa 4:00 jioni saa za Afrika Mashariki, mwishoni ikawa tarehe Machi 20, 2021.

Tuzo na uteuzi[hariri | hariri chanzo]

Mwaka Kazi iliyoteuliwa Tuzo Matokeo
2020 Mwigizaji bora wa kike Yasmin Said Ameshinda [7]
Kipindi bora cha televisheni Maria [7]
Mwigizaji bora wa kiume Brian Ogana Ameteuliwa [7]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Maria (TV series)", Wikipedia (in English), 2021-04-18, retrieved 2021-04-20 
  2. Victor Otengo (2021-03-18). Brian Ogana emotionally says goodbye to fans after conclusion of Maria TV show (en). Tuko.co.ke - Kenya news.. Iliwekwa mnamo 2021-04-20.
  3. Victor Ongaya (2020-05-01). Citizen TV Maria cast: Actors and actresses full names and photos (en). Tuko.co.ke - Kenya news.. Iliwekwa mnamo 2021-04-20.
  4. Maria Citizen TV Full Cast & their Real Names, Age, Synopsis, Producers and Writers | Jambo News (en-US). Jalada kutoka ya awali juu ya 2021-04-20. Iliwekwa mnamo 2021-04-20.
  5. Zadock Thomas (2020-05-17). Citizen TV's Maria Plot, Full Cast, Characters and Their Real Names 2021 (en-GB). The East African Feed. Iliwekwa mnamo 2021-04-20.
  6. Samuel Gitonga. Citizen TV Dominates Entertainment Time Slots in Latest Rankings (en-US). Iliwekwa mnamo 2021-04-20.
  7. 7.0 7.1 7.2 Victor Otengo (13 December 2020). Yasmin Said and Sarah Hassan among big winners at Kalasha Awards. Tuko.co.ke. Iliwekwa mnamo 20 April 2021.
Makala hii kuhusu kipindi fulani cha televisheni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Maria (Kipindi cha televisheni) kama waigizaji wake, hadithi au matoleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.