Nenda kwa yaliyomo

Marcel Pagnol

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kigezo:Tfm

Marcel Pagnol
240px-Marcel Pagnol 1931.jpg
Notable work(s)Marius
Jean de Florette
Manon des sources
La Gloire de mon père
Le Château de ma mère

marcel-pagnol.com

Marcel Pagnol (kwa Kifaransa hutamkwa (French pronunciation: [maʁsɛl paɲɔl]; 28 Februari 1895 – 18 Aprili 1974) alikuwa mwandishi wa vitabu, mwandishi wa tamthilia na mtunzi wa filamu kutoka nchini Ufaransa. Mnamo mwaka 1964, alikua mtunzi wa filamu wa kwanza kuchagulia kujiunga na Académie Française.

Wasifu[hariri | hariri chanzo]

Pagnol alizaliwa tarehe 28 Februari 1895 sehemu iitwa Aubagne, iliyoko kusini mwa Ufaransa. Akiwa mtoto mkubwa kati ya watoto wa mwalimu aliyefahamika kwa jina la Joseph Pagnol A and seamstress Augustine Lansot.B[1] Marcel Pagnol alikua katika mji wa Marseille akiwa na wadogo zake Paul, Rene na dada yake mdogo aliyefahamika kwa jina la Gernaine.

Akiwa shuleni[hariri | hariri chanzo]

Karika hali ya mshangao, hasa kwa baba yake, Pagnol, aliweza kufahamu kusoma akiwa katika umri mdogo. .[onesha uthibitisho] . Hata hivyo mama yake hakumruhusu kushika kitabu hadi alipofikisha umri wa miaka sita, akiogopa kupatwa na ugonjwa wa akili. Mnamo mwezi wa saba mwaka 1904, familia yake alikua katika maadhimisho ya sherehe zilizofahamika kama Bastide Neuve [1] – iliyofanyika katika kijiji kimoja cha La Treille – katika sikukuu za majira ya joto, ambapo watu wengi huyatumia wakiwa katika milima ya Aubagne na Marseille.[2] . Akiwa karibia na umri ule ule, afya ya Augustine ambayo haikuwahi kutengemaa, ilianza kuwa mbaya kwa mara nyingine, na hatimaye tarehe 16 Juni 1910, alipata maambukizi ya kifua na baadae kufariki akiwa na umri wa miaka 36. [3] Joseph alioa kwa mara nyingine mwaka 1912. [1] . Mwaka 1913, akiwa na umri wa miaka 18, Marcel alifaulu katika mitihani yake ya filosofia na hatimaye akajiunga na chuo kikuu cha Aix-en-Provice na kuchukua masomo ya maandiko. Wakati Vita vya Pili vya Dunia vilipoibuka, aliitwa kwenda kufanya kazi lakini baadae aliachiwa kuondoka kutoka na hali yake kutokua nzuri. Tarehe 2 Machi 1916, alimuoa Simone Colin katika eneo la Marseille na mwezi Novemba alifanikiwa kuhitimu katika mafunzo ya Kiingereza.[1] na kuwa mwalimu wa kiingeza katika shule mbalimbali katika eneo lao hasa katika eneo la lycée lililopo Marseille.[1]

Paris: Mwalimu na Mwandishi wa tamthiliya[hariri | hariri chanzo]

Mwaka 1922, alihamia katika jiji la Paris ambapo alikua akifundisha kiingereza hadi mwaka 1927 ,[1] ambao aliamua kujitolea maisha yake kwa ajili ya kuandika michezo ya kuigiza au tamthilia. Katika kipindi hili alikua akifanya kazi na kundi dogo la waandishi , ambapo baadae alishirikiana na mmoja wao aliyefahamika kwa jina la Paul Nivoix ambapo waliandika tamthilia ya Merchants of Glory ambayo iliweza kuzalishwa mwaka 1924. [1] . Baadae aliamua kuondoka katika mji wa Paris na kurejea katika eneo alilozaliwa ambapo aliendelea kutunfa tamthilia mbalimbal ikiwamo ile ya Marius ambayo baadae ilikuja kuwa filamu yake ya kwanza iliyotoka mwaka 1921 Akiwa yupo mbali na Simone Collin (mkewe wa pili) japokuwa ilikuwa si kwa talaka hadi 1941, alianzisha uhusiano na mchezaji muziki wa kiingereza aliyefahamika kama Kitty Murphy, na kupata mtoto mmoja aluyeitwa Jacques Pagnol, aliyezaliwa tarehe 24 Septermber 1930.[1] (Jacques later became his father's assistant and subsequently a cameraman for France 3 Marseille.)

Utunzi wa filamu[hariri | hariri chanzo]

Mnamo mwaka 1926, akiwa katika matembezi katika jiji la London, Pagnol alitembelea moja kati ya nyumba za sinema na kufanikiwa kuona sinema iliyokua na umaarufu sana na hivyo aliamua kutoa muda wake mwingi katika utunzi wa filamu. Hapo, aliwasiliana na studio za Paramount Picture na kupendekeza kuwa kitabu chake cha tamthilia kilichofahamika kama Marius kiweza kufanywa katika filamu. Baadae filamu ilitengenezwa, ikaongozwa na Alexander Korda na kutoka tarehe 10 Oktoba 1931. Ilifanikiwa kuwa moja kati ya filamu za kifaransa zilizopata umaarufu mkubwa sana. Miaka iliyofuatia aliendelea kutengeneza filamu nyingi zake binafsi huku yeye alichukua nafasi mbalimbali katika utengenezaji wake kama vile, mbongozaji picha, mwandishi wa mazungumzo au mkalimani.

Mwandishi wa vitabu vya hadithi[hariri | hariri chanzo]

Mwaka 1945, Pagnol alioa kwa mara nyingine, mwigiziaji Jacquline Bouvier [1] ambapo walipata watoto wawili pamoja, Frederic aliyezaliwa mwaka 1946, na Estelle aliyazaliwa mwaka 1949. Estelle alifariki akiwa na miaka miwili, Pagnol aliumia na kuamia kuhama katika eneo hilo na kurudi Paris. Aliendelea kuandika tamthilia, lakini hazikuweza kufanya vizuri katika masoko na hivyo kuamua kuanza kuandika vitabu vya wasifu. Pagnol alifariki dunia Paris, Aprik 18, 1974.[1] na amezikwa katika makaburi ya Marseille pamoja na mama, baba, kaka na mke wake.

Tuzo[hariri | hariri chanzo]

  • 1939: Best foreign film for HARVEST - New York Film Critics Circle Awards
  • 1940: Best foreign film for The Baker's Wife - New York Film Critics Circle Awards
  • 1950: Best foreign film for Jofroi - New York Film Critics Circle Awards

Wasifu[hariri | hariri chanzo]

Filamu (kama mwandishi, mwongozaji na mzalishaji[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • ^A  Born 25 Oktoba 1869. Died 8 Novemba 1951, age 82.
  • ^B  Born 11 Septemba 1873. Died 16 Juni 1910, age 36.
  1. 1.00 1.01 1.02 1.03 1.04 1.05 1.06 1.07 1.08 1.09 Castans (1987), pp. 363–368
  2. Castans (1987), p. 22.
  3. Castans (1987), pp. 27, 32.
  4. Manon des Sources (1952 film) katika Internet Movie Database

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Alitanguliwa na
Maurice Donnay
Seat 25
Académie française

1946–74
Akafuatiwa na
Jean Bernard