Nenda kwa yaliyomo

Mara tatu-mbili

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Mara tatu-mbili (Triple-double) kweye mpira wa kikapu ni uchezaji wa mchezo mmoja unaofanywa na mchezaji ambaye hukusanya jumla ya tarakimu mbili katika kategoria tatu kati ya tano za takwimupointi, mipira iliyorudi, pasi za bao(asisti), mipira ilioibiwa au ilioibwa na mipira iliozuiliwa—katika mchezo mmoja. Njia ya kawaida ya mchezaji kufikia mara tatu-mbili ni kwa pointi, mipira inayorudi , na pasi za mabao(asisti), ingawa wakati fulani wachezaji wanaweza kuweka rekodi ya kuiba mipira 10 au zaidi au kuzuia mipira katika mchezo.[1] Asili ya neno "Mara tatu-mbili" haipowazi. Vyanzo vingine vinadai kuwa ilibuniwa katika Chama Cha Mpira wa Kikapu Marekani (NBA) na aliyekuwa mkurugenzi wa mahusiano ya umma wa Los Angeles Lakers Bruce Jolesch katika miaka ya 1980 ili kuonyesha uwezo mwingi wa Magic Johnson,[1][2] huku wengine wakidai kuwa ilibuniwa na mkurugenzi wa mahusiano ya vyombo vya habari vya Philadelphia 76ers Harvey Pollack mwaka wa 1980.[3]

  1. "They're Vintage Triple-Doubles - Los Angeles Times". web.archive.org. 2012-10-13. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-10-13. Iliwekwa mnamo 2023-05-21.
  2. "USA Today", Wikipedia (kwa Kiingereza), 2023-05-17, iliwekwa mnamo 2023-05-21
  3. "Philly's Pollack has kept track of NBA from the start - USATODAY.com". web.archive.org. 2012-10-26. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-10-26. Iliwekwa mnamo 2023-05-21.