Nenda kwa yaliyomo

Mambo Mambo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
“Mambo Mambo”
“Mambo Mambo” cover
Single ya Lou Bega
kutoka katika albamu ya A Little Bit of Mambo
Imetolewa 5 Juni 2000
Muundo CD single
Aina Pop ya Kilatini, Mambo
Urefu 3:00 (toleo halisi)

3:17 (toleo la redio)

Studio Lautstark / BMG / RCA Records
Mtunzi Lou Bega
Zippy Davids
Frank Lio
Donald Fact
Mtayarishaji Goar B
Frank Lio
Donald Fact
Mwenendo wa single za Lou Bega
"Tricky, Tricky"
(1999)
"Mambo Mambo"
(2000)
"Gentleman"
(2001)

"Mambo Mambo" ni single ya nne ya mwanamuziki wa Kijerumani - Lou Bega. Single inatoka katika albamu ya A Little Bit of Mambo. Imekuja kuwa kibao pekee katika chati za Single za Kifaransa ambamo ilishisha nafasi ya 11 na pia katika chati za Walloon singles chart ambao pia ilishika nafasi ya 25.

Mashairi

[hariri | hariri chanzo]

Wimboni anazungumzia rabsha mbalimbali za starehe na mwanamke aliyeitwa Mambo. Isichanganywe na mambo ya Kiswahili. Anasema anacheza Rumba, Salsa, Chacha, Limbo, Foxtrott hata Tango akiwa na wasichana, wamama na watoto huku DJ akipiga wimbo huu maadamu upo katika orodha ya nyimbo zao za kuchezwa. Hajaishia hapo. Akasema katika safari yake, kupitia dansi hili amekutana na mambo mazuri ya kufurahisha nafsi. Lakini Mambo anamshangaza na kuduwaza na hatimaye akamwachia kwa huba la nguvu.

Hivi ndivyo anavyokwenda na Mambo Mambo eh.

Muundo wa mashairi ni kuwarudia yaleyale aliyosema hapo awali, lakini katika mtindo usiochusha.

Orodha ya nyimbo

[hariri | hariri chanzo]
CD single
  1. "Mambo Mambo" (Toleo la Redio) - 3:17
  2. "Baby Keep Smiling" (Toleo la Albamu) - 3:10


Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]